VIDEO: Daraja kubwa marekani kukatika na kuporomoka

VIDEO: Daraja kubwa marekani kukatika na kuporomoka

VIDEO: Daraja kubwa marekani kukatika na kuporomoka – Watu wapatao 20 wanasadikika kutumbukia kwenye maji baada ya daraja la Francis Scott lililopo Baltimore Nchini Marekani kukatika vipandevipande leo March 26,2024 baada ya meli iliyobeba kontena kuligonga.

Boti kadhaa za Vikosi vya uokoaji zimeonekana kwenye Mto huo uitwao Patapaco wakiwemo Wazamiaji ambao wamekiri kuwa magari kadhaa yameonekana kwenye maji.

Daraja hilo la kilometa 2.5 ni kiungo muhimu kwa Watumiaji mbalimbali wa eneo hilo ambapo meli hiyo inayopeperusha bendera ya Singapore imetajwa kuwa na urefu wa futi 948 kwenda juu.

Mji wa Baltimore uliopo ndani ya Jimbo la Maryland ni Mji wenye Wakazi zaidi ya laki tano kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2020 na ni nyumbani wanakotoka Mastaa kama Jada Pinkett Smith, Sisqó, Mwimbaji Marioo na Spika aliyepita Nancy Pelosi.

See also;