Vijue vyakula vya kuongeza nguvu za kiume

Vijue vyakula vya kuongeza nguvu za kiume, Nguvu za kiume ni nguvu au uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa. Upungufu wa nguvu za kiume hutofautiana baina ya mtu mmoja na mwingine. Tatizo hili linaweza kuwa ni kushindwa kusimamisha uume (uume kutosimama vizuri) au hali ya kufika kileleni haraka kabla ya wakati, hivyo kutomridhisha mwenza wako.

Pamoja na hayo wanaume wanaume tunatakiwa kutambua tendo hili hulinda na kuleta heshima ya ndoa, Leo hii nakusegezea elimu hii ya vitu vitakavyo linda ndoa/mahusiano yako

Vijue vyakula vya kuongeza nguvu za kiume

Tiba Asili za Kuimarisha Nguvu za Kiume, Hapa kuna njia mbalimbali za asili za kusaidia kuimarisha nguvu za kiume na kutatua matatizo yanayohusiana na upungufu wa nguvu za kiume:

  1. Kitunguu Swaumu

    • Tumia punje 8-10 za kitunguu swaumu zilizomenywa na kukatwakatwa vipande vidogo vidogo. Meza na glasi mbili za maji safi na salama, mara mbili kwa siku (asubuhi na jioni) kwa muda wa mwezi mmoja. Pia, hakikisha unatumia kitunguu swaumu kama kiungo katika chakula chako, ukikiweka mwishoni ili kisiive sana na moto.
  2. Tikiti Maji

    • Kula tikiti maji kila siku huku ukitafuna na mbegu zake. Fanya hivyo siku zote kwa afya bora ya nguvu za kiume.
  3. Ugali wa Dona

    • Kula ugali wa dona badala ya ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi muhimu kwa afya ya mwanaume. Kama ugali wa dona una kukera, changanya mahindi kilo 10 na ngano kilo 3, usage pamoja. Ugali wake huwa mlaini, mzuri, na mtamu. Kula na mboga yoyote.
  4. Chumvi ya Mawe

    • Tumia chumvi ya mawe ya bahari, ambayo haijasafishwa wala kupitishwa kiwandani, kwenye vyakula vyako kila siku. Ina mchango mkubwa katika kutibu tatizo hili.

      Vijue vyakula vya kuongeza nguvu za kiume
      Vijue vyakula vya kuongeza nguvu za kiume
  5. Maji ya Kunywa

    • Kunywa maji ya kutosha kila siku bila kusubiri kiu. Kila mtu anahitaji glasi 8-10 za maji kwa siku. Maji ni muhimu katika kuongeza damu, kuimarisha mwili, na kutoa taka mwilini.
  6. Mbegu za Maboga

    • Ziloweke katika maji yenye chumvi, zikaushe kisha zikaange kidogo bila kuziunguza. Tafuna mbegu 100 mara 3 kwa siku kwa muda wa mwezi mmoja. Mbegu hizi zinaongeza wingi wa mbegu za kiume (manii) na ni muhimu kwa wale wenye tatizo la kutoa manii machache (low sperm count).
  7. Asali na Mdalasini

    • Chukua lita moja ya asali safi ya asli ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 4 vya mdalasini ya unga, changanya vizuri pamoja. Lamba kijiko kimoja kikubwa kila unapokwenda kulala. Fanya hivi kwa mwezi mmoja.
  8. Chai ya Tangawizi

    • Tangawizi husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini na husukuma damu kwenda kwenye viungo vya uzazi (uke na uume). Unaweza kutafuna tangawizi mbichi, kupika au kuianika na kuitumia kama unga.

SEE ALSO: