KIKOSI cha Yanga Kilichosafiri Kwenda Ethiopia Leo

KIKOSI cha Yanga Kilichosafiri Kwenda Ethiopia Leo | Kikosi cha Young Africans SC (Yanga) kimewasili Ethiopia mapema leo, likiwa tayari kwa maandalizi ya mchezo muhimu dhidi ya CBE SA. Mchezo huu ni sehemu ya michuano ya hatua za awali za Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) na utafanyika Jumamosi, Septemba 14, 2024, katika Uwanja wa Abebe Bikila, jijini Addis Ababa.

Msafara wa timu hiyo umejumuisha jumla ya watu 36, wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi, na viongozi mbalimbali wa klabu. Yanga imeweka kambi na inatarajiwa kufanya mazoezi ya mwisho kesho kabla ya kuingia uwanjani kwa lengo la kupata matokeo mazuri ugenini.

Mchezo huo utarushwa moja kwa moja (LIVE) kupitia AzamSports2HD kuanzia saa 9:00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki. Mashabiki wa Yanga na wapenzi wa soka nchini Tanzania wataweza kufuatilia moja kwa moja hatua za timu yao kwenye kinyang’anyiro hiki cha kimataifa, wakitarajia ushindi ili kujipatia faida ya kufuzu kwa hatua zinazofuata.

KIKOSI cha Yanga Kilichosafiri Kwenda Ethiopia Leo

KIKOSI cha Yanga Kilichosafiri Kwenda Ethiopia Leo
KIKOSI cha Yanga Kilichosafiri Kwenda Ethiopia Leo

Matarajio ni kwamba Yanga itawakilisha vyema Tanzania na kuonyesha kiwango bora katika michuano hii mikubwa ya bara la Afrika.

ANGALIA PIA: