Antony Kagoma Kuondoka Man UTD, Ataka muda zaidi

Antony Kagoma Kuondoka Man UTD, Ataka muda zaidi | Winga wa Manchester United, Antony, amejitokeza na kukataa kuondoka klabuni licha ya ripoti za awali kueleza kuwa klabu hiyo ilikuwa kwenye mazungumzo ya kumuuza. Antony, ambaye ana umri wa miaka 24, amewaambia mabosi wa Manchester United kwamba anahitaji kupambania nafasi yake katika kikosi cha kwanza.

Awali, iliripotiwa kwamba Manchester United ilikuwa inajadili na klabu ya Fenerbahce kuhusu uwezekano wa kumuuza Antony kama sehemu ya mpango wa kupunguza matumizi ya klabu. Antony alisajiliwa na Manchester United kwa ada kubwa, na kuwa mmoja wa wachezaji ghali zaidi kwenye kikosi cha Mashetani Wekundu.

Msimu huu, Antony amecheza mechi moja tu kwenye Ligi Kuu ya England, ambapo alitokea benchi na kuingia kucheza dakika moja. Hata hivyo, ameonyesha dhamira ya kuendelea kupambania nafasi yake na kusalia kwenye timu, licha ya changamoto zinazomkabili.

Antony Kagoma Kuondoka Man UTD, Ataka muda zaidi

Antony Kagoma Kuondoka Man UTD, Ataka muda zaidi

ANGALIA PIA: