Lil Wayne Aeleza Kutochaguliwa Kuongoza Super Bowl Halftime Show

Lil Wayne Aeleza Kutochaguliwa Kuongoza Super Bowl Halftime Show | Rapa maarufu Lil Wayne ameweka wazi hisia zake kuhusu kutopata nafasi ya kuongoza orodha ya wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Super Bowl Halftime Show. Lil Wayne ameeleza kuwa kitendo hicho kimemuumiza na kwamba hakuwa tayari kiakili kupokea taarifa hiyo, akitarajia kupata nafasi hiyo kutokana na mchango wake mkubwa kwenye tasnia ya muziki.

Hivi karibuni, waandaaji wa tamasha hilo walimtangaza Kendrick Lamar kama msanii mkuu (‘headliner’) wa onyesho hilo kubwa, uamuzi ambao umeibua mijadala miongoni mwa mashabiki na wasanii. Baadhi ya wasanii maarufu, akiwemo Nicki Minaj na Master P, wameeleza kutoridhishwa kwao na uamuzi huo, wakihisi kwamba Lil Wayne alistahili nafasi hiyo kutokana na mafanikio na ushawishi wake kwenye muziki wa rap kwa muda mrefu.

Lil Wayne Aeleza Kutochaguliwa Kuongoza Super Bowl Halftime Show
Lil Wayne Aeleza Kutochaguliwa Kuongoza Super Bowl Halftime Show

Ingawa Kendrick Lamar ni msanii anayeheshimika sana, mjadala huu umeweka wazi kwamba baadhi ya mashabiki na wasanii walikuwa na matarajio makubwa ya kumwona Lil Wayne kwenye jukwaa hilo la hadhi kubwa.

ANGALIA PIA: