Ratiba ya Wasafi Festival 2024

Ratiba ya Wasafi Festival 2024 | Msanii maarufu wa Bongofleva, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’, amezindua msimu mpya wa Wasafi Festival 2024 kwa kishindo, akihudhuriwa na wasanii mbalimbali pamoja na viongozi wa serikali. Uzinduzi huo ulifanyika kwa sherehe kubwa, ukiashiria mwanzo wa msimu wa burudani unaotarajiwa kuwaburudisha mashabiki wake kote nchini.

Diamond Platnumz, akiwa kinara wa muziki wa Bongofleva, amekuwa akiutumia Wasafi Festival kama jukwaa la kuibua vipaji vipya na kuimarisha nafasi yake katika tasnia ya burudani nchini na kimataifa.

Hata hivyo, siku si nyingi baada ya uzinduzi huo wa Wasafi Festival, msanii mwenzake Nandy, anayejulikana kwa umahiri wake katika muziki wa Bongofleva, naye amezindua tamasha lake la Nandy Festival 2024.

Tamasha hili la Nandy linaonesha ushindani mzuri kati ya wasanii hawa wawili wakubwa, huku wote wakilenga kutoa burudani ya kiwango cha juu kwa mashabiki wao nchini na kimataifa. Nandy Festival imekuwa ni jukwaa muhimu kwa msanii huyo kuonesha mafanikio yake ya kimuziki na kutoa fursa kwa wasanii wengine chipukizi kuonesha vipaji vyao.

Ratiba ya Wasafi Festival 2024

Ratiba ya Wasafi Festival 2024
Ratiba ya Wasafi Festival 2024

Msimu huu wa 2024 unaonekana kuwa wa ushindani mkubwa katika tasnia ya burudani, huku wasanii wa Bongofleva wakiendelea kutoa burudani ya kipekee na ya kusisimua.

ANGALIA PIA: