Al Ahly Yaanza kwa Ushindi Dhidi ya Gor Mahia

Al Ahly Yaanza kwa Ushindi Dhidi ya Gor Mahia | Mchezo wa kufuzu hatua ya makundi CAF Champions League/Kalabu Bingwa Afrika kati ya Al Ahly vs Gor Mahia.

Al Ahly Yaanza kwa Ushindi Dhidi ya Gor Mahia

AL-AHLY imeibuka na ushindi wa kwanza wakiwa ugenini katika mchezo wa kufuzu hatua ya makundi klabu bingwa msumu huu, mchezo uliochezwa Kenya kwenye uwanja wa nyumbani wa Gor Mahia.

Kabla ya mchezo huu kulikuwa na minong’ono kwamba Al Ahly kufanyiwa figisi kuelekea mchezo huu ili kuipa faida ya nyumbani timu ya mpira ya Gor Mahia, licha ya maneno mengi Al Ahly kaonyesha ukubwa wake kwenye mchezo huo na kuibuka na ushindi mnono wa goli 3-0.

Magoli ya Al Ahly yamefungwa na wachezaji Ramy Rabia na Percy Tau, hadi kipindi cha kwanza kinatamatika Al Ahly alikuwa akiongoza kwa goli 2-0. Goli la tatu limefungwa kipindi cha pili na Percy Tau na kuitimisha ushindi wa goli 3. Mpira ukatamatika kwa kushuhudia Gor Mahia wakipoteza kwa ushindi wa 3-0 (Gor Mahia 0-3 Al Ahly )

Al Ahly Yaanza kwa Ushindi Dhidi ya Gor Mahia
Al Ahly Yaanza kwa Ushindi Dhidi ya Gor Mahia

PICHA YA KUFUZU

Mpaka sasa Al Ahly ananafasi kubwa ya kusonga mbele hatua ya makundi kutokana na mtaji mkubwa wa magoli waliyopata kwenye mchezo wa ugenini leo. Hivyo mchezo wa Cairo unaweza kuwa mwepesi sana kwao na uwezekano wa kushinda pia ni mkubwa kwa upande wao, hivyo asilimia 80 mpaka sasa AL AHLY amefuzu hatua ya makundi.

Gor Mahia wana asilimia chache za kufuzu lakini inategemea zaidi na juhudi watakayo iweka kuelekea mchezo unaofuata, ni vyema wakasahau matokeo ya leo na kujiimarisa zaidi kimbinu ili waweze pata matokeo mazuri kwenye mchezo wa marudiano.

ANGALIA PIA: