Shughuli za Sanaa Kusimamishwa Kupisha Maulid Zanzibar

Shughuli za Sanaa Kusimamishwa Kupisha Maulid Zanzibar

Shughuli za Sanaa Kusimamishwa Kupisha Maulid Zanzibar | Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni (BASSFU) limetangaza kusitisha shughuli zote za sanaa na burudani nchini Tanzania kwa muda ili kupisha usiku wa mkesha wa Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W), utakaoadhimishwa Jumapili, tarehe 15 Septemba 2024.

Taarifa hiyo imetolewa kwa mujibu wa Sheria Na. 7 ya Mwaka 2015, ambayo inawapa mamlaka BASSFU kusimamia na kudhibiti shughuli zote zinazohusiana na sanaa, filamu, na utamaduni nchini.

Katika taarifa hiyo, taasisi au mtu yeyote atakayekaidi agizo hilo, atachukuliwa hatua kali za kisheria. Sheria hii inawahusu wasanii, waendeshaji wa kumbi za burudani, na sehemu zote zinazotoa huduma za burudani na sanaa ili kutoa heshima kwa siku hii takatifu.

Shughuli za Sanaa Kusimamishwa Kupisha Maulid Zanzibar

Kwa hivyo, shughuli zote za burudani nchini, ikiwemo muziki, filamu, na matamasha ya sanaa, zitasitishwa kwa kipindi hicho hadi siku itakapopita.

ANGALIA PIA: