Kocha wa KenGold Fikirini Bakari Afikiria Kujiuzulu Baada ya Kichapo Dhidi ya KMC

Kocha wa KenGold Fikirini Bakari Afikiria Kujiuzulu Baada ya Kichapo Dhidi ya KMC | Mara baada ya timu yake, KenGold FC, kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya KMC FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, kocha Fikirini Bakari ameweka wazi kuwa anafikiria kujiuzulu nafasi yake kama kocha mkuu.

Fikirini alieleza kuwa ameshindwa kufikia malengo aliyokuwa amepanga na timu hiyo, na sasa ni wakati wa kujitathmini na kuona kama hatua bora ni kuachia nafasi hiyo kwa mtu mwingine.

Kocha Fikirini aliongeza kuwa, licha ya jitihada zake kujaribu kubadilisha mwenendo wa timu, matokeo yamekuwa si mazuri kama alivyotarajia. Kwa hiyo, kama sehemu ya uwajibikaji na heshima kwa timu, anaona busara kufikiria kujiuzulu ili kumpisha kocha mwingine kuendeleza jitihada za timu.

Hali hii inafuatia mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha kwa KenGold FC, ambao kwa sasa wanakabiliwa na presha ya kuboresha nafasi yao katika ligi.

Kocha wa KenGold Fikirini Bakari Afikiria Kujiuzulu Baada ya Kichapo Dhidi ya KMC

Kocha wa KenGold Fikirini Bakari Afikiria Kujiuzulu Baada ya Kichapo Dhidi ya KMC

“Hadi sasa nipo nje ya malengo, mimi kama mwalimu napaswa kujitathimini, nafikiria bora nikae pembeni nijitathimini na hii inaweza ikawa ndio mechi yangu ya mwisho.”- Fikiri Elias Head Coach KenGold FC.

ANGALIA PIA: