Joash Onyango Akanusha Kuondoka Simba Kwa Shinikizo Lake

Joash Onyango Akanusha Kuondoka Simba Kwa Shinikizo Lake

Joash Onyango Akanusha Kuondoka Simba Kwa Shinikizo Lake | Mlinzi wa Klabu ya Dodoma Jiji, Joash Onyango, amejitokeza na kukanusha ripoti zilizosambaa zikidai kuwa yeye ndiye aliyesababisha kuondoka kwake kutoka Klabu ya Simba msimu uliopita. Onyango, ambaye aliunda pacha thabiti na beki mwenzake Pascal Wawa akiwa Simba, amesema hajawahi kushinikiza kuondoka kwenye klabu hiyo.

Akitolea ufafanuzi suala hilo, Onyango alieleza kuwa hakuwahi kuomba kuachana na Simba, badala yake, ni uongozi wa klabu hiyo ya soka ya Dar es Salaam uliamua kumruhusu kuondoka. Beki huyo wa kimataifa wa Kenya aliongeza kuwa uamuzi huo ulifanywa na viongozi wa Simba bila yeye kuwa na ushawishi wowote katika suala hilo.

Joash Onyango Akanusha Kuondoka Simba Kwa Shinikizo Lake

Onyango aliondoka Simba baada ya kipindi cha mafanikio makubwa akiwa sehemu muhimu ya safu ya ulinzi ya klabu hiyo, na sasa amejiunga na Dodoma Jiji ambapo anajitahidi kuendeleza uwezo wake wa kucheza soka.

ANGALIA PIA: