Yanga Kuwakabili CBE Uwanja wa Amaan Complex Jumamosi

Yanga Kuwakabili CBE Uwanja wa Amaan Complex Jumamosi

Yanga Kuwakabili CBE Uwanja wa Amaan Complex Jumamosi | Yanga SC Dhidi ya CBE SA Uwanja wa Amaan Complex Jumamosi katika Mechi ya Marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Jumamosi hii, Yanga SC watakuwa uwanja wa Amaan Complex, Zanzibar, kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya CBE SA ya Ethiopia, katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mchezo huu utapigwa kuanzia saa 2:30 usiku na utaonyeshwa moja kwa moja kupitia AzamSports1HD.

Yanga Kuwakabili CBE Uwanja wa Amaan Complex Jumamosi
Yanga Kuwakabili CBE Uwanja wa Amaan Complex Jumamosi

Wananchi (Yanga SC) wanasonga mbele katika mchezo huu wakiwa na faida ya ushindi wa goli moja, walilopata kwenye mechi ya kwanza iliyochezwa Addis Ababa, ambapo walishinda 1-0. Ushindi huo unawapa nafasi nzuri kuelekea mechi ya nyumbani, lakini watatakiwa kuwa makini kuhakikisha wanaendeleza ubora wao ili kusonga mbele kwenye hatua ya makundi ya mashindano hayo ya kifahari barani Afrika.

Mashabiki wa Yanga SC wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kuipa timu yao sapoti katika uwanja wa Amaan, wakilenga kuona timu yao ikipata ushindi mwingine na kufuzu kwa hatua inayofuata.

ANGALIA PIA: