Makundi ya CAF Klabu Bingwa Africa 2024/2025, Champions League Groups

Makundi ya CAF Klabu Bingwa Africa 2024/2025, Champions League Groups | Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika, limetangaza makundi ya Klabu Bingwa Afrika (CAF Champions League) kwa msimu wa 2024/2025. Hafla hiyo iliyosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka barani kote, imefanyika jijini Cairo, Misri, ambapo vilabu bora vya Afrika vilivyofuhu hatua ya makundi vilipangwa katika makundi rasmi ya michuano hii mikubwa ya vilabu barani.

Msimu huu, mashindano ya Klabu Bingwa Afrika yanatarajiwa kuwa na ushindani mkali, huku timu zinazoshiriki zikiwa na rekodi nzuri katika soka la kimataifa. Kila kundi limeleta changamoto za kipekee, na mashabiki wanaweza kujiandaa kwa mechi zenye mvuto na ushindani mkubwa zitakazowakutanisha mabingwa wa zamani na timu zinazoibuka kwa kasi.

Baada ya droo hii, wachambuzi wa soka wameanza kutoa maoni yao kuhusu makundi, huku wengi wakitabiri kuwa Kundi A litakuwa “kundi la kifo” kutokana na uwepo wa timu ambazo zipo katika kiwango bora kama Yanga sc, Tp Mazembe na Al Hilal SC. Hata hivyo, michuano hii imekuwa na misukosuko mingi hapo awali, na hakuna anayeweza kutabiri kwa uhakika ni timu gani itaibuka kidedea

Makundi ya CAF Klabu Bingwa Africa 2024/2025, Champions League Groups

Haya hapa makundi ya Klabu Bingwa Afrika CAF kwa msimu wa 2024-25:-

  • Kundi A:
    • TP Mazembe (DR Congo)
    • Young Africans (Tanzania)
    • Al Hilal SC (Sudan)
    • MC Alger (Algeria)
  • Kundi B:
    • Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
    • Raja CA (Morocco)
    • ASFAR Club (Morocco)
    • AS Maniema Union (DR Congo)
  • Kundi C:
    • Al Ahly FC (Misri)
    • CR Belouizdad (Algeria)
    • Orlando Pirates (Afrika Kusini)
    • Stade d’Abidjan (Ivory Coast)
  • Kundi D:
    • ES Tunis (Tunisia)
    • Pyramids FC (Misri)
    • Sagrada Esperança (Angola)
    • Djoliba AC de Bamako (Mali)

ANGALIA PIA: