Sifa za Mashairi ya Kisasa: Shairi ni aina ya fasihi. Mashairi ni tungo zenye kutumia mapigo ya silabi kwa utaratibu maalumu wa kimuziki kwa kutumia lugha ya mkato, lugha ya picha na tamathali za semi.
Kuna mashairi yanayofuata taratibu za kimapokeo, yaani yanazingatia taratibu za urari na vina, mizani, idadi sawa ya mistari, vituo na beti. Mashairi hayo huwa na mizani 14 au 16 katika kila mstari, yaani mizani 7 au 8 kwa kila kipande cha mstari.
Kuna mashairi yanayofuata taratibu za kimapokeo, yaani yanazingatia taratibu za urari na vina, mizani, idadi sawa ya mistari, vituo na beti. Mashairi hayo huwa na mizani 14 au 16 katika kila mstari, yaani mizani 7 au 8 kwa kila kipande cha mstari.
Pia kuna mashairi yasiyofuata utaratibu huo wa kimapokeo na huitwa mashairi ya kimamboleo. Mashairi hayo mara nyingi ni nyimbo.
Sifa za Mashairi ya Kisasa
Aina za mashairi
Kwenye Sifa za Mashairi ya Kisasa Kuna aina kuu mbili za ushairi, nazo ni kama zifuatazo:
(i) Ushairi wa kimapokeo
Haya ni mashairi yanayozingatia kanuni za mizani/mizani (ulinganifu), maudhui, idadi ya mishororo katika kila ubeti na katikati katika shairi. Pia huitwa mashairi yaliyofungwa.
Aina ya ushairi kulingana na mtindo huu wa mapokeo, hupatikana kwa kuangalia idadi ya mishororo katika kila ubeti kwenye Sifa za Mashairi ya Kisasa.
(ii) Ushairi huru
Haya ni mashairi yasiyofuata kanuni za kimapokeo, yaani hayafuati kanuni za mizani/mizani (ulinganifu), yana idadi ya mishororo katika kila ubeti na katikati katika shairi. Mashairi haya pia huitwa mashairi ya ghuni/mashairi ya kisasa/masivina/mapingiti.
Mizani
Mizani ni uwiano wa idadi ya silabi katika kila ubeti au mstari wa shairi. Mashairi mengi ya kimapokeo yana vina nane (8) kwa kila ubeti na vina kumi na sita (16) kwa kila mstari (mshororo). Vilevile katika mashairi mengine, kuna mizani saba (7) kwa kila kipande huku kila mstari una mizani kumi na nne (14).
Vina
Vina ni silabi zenye sauti sawa zinazotokea katikati au mwisho wa kila mstari wa kila ubeti wa shairi. Kwa hivyo kuna za kati na za mwisho.
Ili shairi lako lihesabiwe kuwa kamili, herufi za mwisho na za kati za ubeti wako lazima zilingane.
Kwenye Sifa za Mashairi ya Kisasa, Mistari ya kati katika kila ubeti lazima iwe sawa, na mistari ya mwisho lazima pia iwe sawa katika ubeti.
See also:
Leave a Reply