Sifa za kusoma kozi ya sheria ngazi ya shahada/degree

Sheria ngazi ya Shahada/Degree

Sifa za kusoma kozi ya sheria ngazi ya shahada/degree Je, unatamani kusoma sheria au kuwa Wakili, Hakimu au Jaji? Hongera! Soma vigezo na mlolongo wote hapa chini.

Shule ya Sheria ya Tanzania (Shule) ilianzishwa kwa Sheria ya Shule ya Sheria ya Tanzania ya 2007. Hatua hii ilikuja kwa sababu wanasheria wanaotaka kuwa wanasheria walihitaji ujuzi wa vitendo ili kutekeleza sheria.

Sifa za kusoma kozi ya sheria ngazi ya shahada/degree, Kabla ya Shule hiyo, wanafunzi walipata mafunzo ya vitendo ya kisheria kupitia programu ya mafunzo kazini inayoendeshwa na Baraza la Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Baadaye baadhi ya vyuo vikuu vilipitisha mfumo unaoitwa wanafunzi wa nje ili kutoa aina hizi hizi za ujuzi wa vitendo. Mifumo hii sasa imebadilishwa na Programu mpya ya Mafunzo ya Kisheria kwa Vitendo inayoendeshwa na Shule iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria.

Sifa za kusoma kozi ya sheria ngazi ya shahada/degree

Sifa za kusoma kozi ya sheria ngazi ya shahada/degree

– Ukitaka kusoma degree ya sheria na umehitimu SECONDARY kidato cha sita (6), unatakiwa uwe umefaulu masomo mawili, kiingereza na historia, uwe walau na “D” mbili na kuendelea.

Na kama hujasoma na kufaulu History na English A – LEVEL (KIDATO CHA SITA), labda umesoma sayansi (PCM, PCB, CBG n.k) au umesoma History na English A Level lakini hujafikisha alama “D” ya masomo hayo, na unatamani kusoma sheria, basi uwe una credit ya history na kiingereza kule O level, yaani uwe umeyafalu kwa kiwango cha alama “C” na kuendelea kule kidato cha nne (4).

NB: Sifa za kusoma kozi ya sheria ngazi ya shahada/degree, Kwa kuwa sasa Kiswahili ni lugha rasmi ya Mahakama na sheria zote zinatakiwa kuandikwa kwa Kiswahili, HUENDA wanaotaka kusoma sheria wakatakiwa kufaulu na kiswahili.

See also: