Sababu za Mwanamke Kukosa Hamu ya Kufanya Mapenzi

Sababu za Mwanamke Kukosa Hamu ya Kufanya Mapenzi: Tatizo la kukosa hamu ya kufanya mapenzi au kukosa nyege kwa lugha ya mitaani huwatokea zaidi wanawake kuliko wanaume, lakini ni wanaume wanaokerwa zaidi na tatizo hili kuliko wanawake.

Wakati ambapo ni asilimia 15 hadi 16 ya wanaume wenye tatizo hili, idadi ya wanawake ni mara mbili ya hii ya wanaume. Lakini wakati ni asilimia 23 ya wanaume wanaonyesha kuridhika kuishi na tatizo hili, asilimia 46 ya wanawake wapo radhi kabisa kuendelea kuishi na tatizo hili.

Si lazima kuendelea kuishi na tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa sababu kuna mambo mengi unayoweza kuyafanya ili kuondokana na hili tatizo.

Hali ya kupenda kufanya mapenzi au tendo la ndoa kwa mwanamke inabadilikabadilika sana ikipanda na kushuka kulingana na matukio mbalibali yanayomtokea katika maisha yake. Baadhi ya matukio yanayoathiri hamu ya mwanamke ya kufanya mapenzi ni pamoja na kuanza na kwisha kwa mahusiano ya kimapenzi na mwanamme, kupata ujauzito, na magonjwa.

Kama wewe mwanamke umepatwa na hali hii unaweza kukabiliana nayo kwa kubalisha jinsi unavyoishi, kufanya mambo kadhaa yatakayobadilisha hali hii au kutumia baadhi ya dawa zinazosaidia kuondoa tatizo hili.

Sababu za Mwanamke Kukosa Hamu ya Kufanya Mapenzi

1. Mahusiano Baina Ya Mwanamke Na Mwanamme

Kwa wanawake walio wengi ukaribu wa kihisia ndicho kitu cha kwanza katika kujenga mapenzi kati yake na mwanamme. Hivyo, mahusiano mabovu yaweza kuwa ndicho chanzo cha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanamke.

Mwanamke atakosa hamu ya kufanya mapenzi endapo hakutokuwa na mawasiliano baina yake na mumewe, kutakuwa na migogoro kati yake na mumewe isiyokwisha, kutakuwa na ukosefu wa mawasiliano kuhusu mahitaji yake ya kufanya mapenzi na jinsi ambavyo yeye angependa kufanyiwa kimapenzi na kama atahisi kuna ukosefu wa uaminifu katika ndoa au mahusiano yao.

2. Matatizo Katika Maisha Yako

Matatizo mbalimbali katika maisha ya mwanamke humsababishia kukosa hamu ya kufanya mapenzi. Baadhi ya matatizo ambayo huweza kusababisha mwanamke kukosa hamu ya kufanya mapenzi ni pamoja na magonjwa, mabadiliko katika mwili wake na hata matumizi ya baadhi ya madawa:

Sababu za Mwanamke Kukosa Hamu ya Kufanya Mapenzi

Matatizo Katika Kufanya Tendo La ndoa.

Kama mwanamke anapata maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa au kama mwanamke anakosa kufika kileleni, hali hii inaweza kusababisha akakosa kabisa hamu ya kufanya mapenzi.

Matatizo ya afya

Magonjwa mengi husababisha mwanamke akose hamu ya kufanya tendo la ndoa. Baadhi ya magonjwa ni maumivu ya viungo vya mifupa (arthritis), kansa, ugonjwa wa kisukari, high blood pressure, matatizo katika mishipa ya damu ya arteri na matatizo ya akili.

Matumizi ya madawa

Baadhi ya madawa yakitumiwa, huondoa kabisa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke. Mfano wa dawa hizo ni madawa ya kukabiliana na msongo wa mawazo.

Mtindo wa maisha

Matumizi ya pombe kuzidi kiwango, uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya huathiri hamu ya kufanya mapenzi.

Upasuaji

Upasuaji uliofanyika katika maeneo ya maziwa au katika maeneo ya viungo vya uzazi humbadilishia mwanamke mwonekano wake, huathiri ufanyaji kazi wa viungo hivyo na mwisho kuathiri hamu yake ya kufanya mapenzi.

Uchovu:

Unaotokana na kulea watoto wadogo au vikongwe huweza kuathiri hamu ya mwanamke ya kufanya mapenzi.

3. Mabadiliko Katika Mfumo Wa Homoni.

Kukoma hedhi: Mabadilko ya viwango vya homoni katika mwili wa mwanamke yanaweza kusababisha kukosa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke. Kupungua kwa Estrogen katika mwili wa mwanamke katika kipindi cha kuelekea kukoma hedhi kunaweza kusababisha ukosefu wa hamu ya kufanya mapenzi. Upungufu wa homoni hiyo husababisha uyabisi wa viungo vya sehemu nyeti na kusababisha maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Mwanamke pia huweza kuwa na upungufu wa homoni ya testosterone, homoni ambayo husaidia kuongeza hamu ya kufanya mapenzi kwa wanaume na wanawake, hivyo mwanamke huyo akapungukiwa na hamu ya kufanya mapenzi.

Pamoja na kuwa wanawake wengi huendelea kupata hamu ya kufanya mapenzi baada ya kukoma hedhi, baadhi kupungukiwa na hamu hiyo baada ya mabadiliko haya ya viwango vya homoni katika miili yao.

Ujauzito na kunyonyesha. Mabadiliko katika mfumo wa homoni wakati wa ujauzito, baada ya kujifungua na wakati wa kunyonyesha huweza kusababisha mwanamke kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.

4. Matatizo Ya Kisaikolojia

Matatizo ya kisaikolojia yana mchango katika kumfanya mwanamke akose hamu ya kufanya tendo la ndoa. Baadhi ya mtatatizo hayo ni:

  1. Wasiwasi na kuwa na msongo wa mawazo
  2. Kuwa na mawazo mengi kuhusu matatizo ya kifedha au kikazi
  3. Kuhisi kutothaminiwa katika jamii
  4. Kuwa na historia ya kunyanyaswa kimwili au kijinsia kama kupigwa au kubakwa
  5. Kuwa na historia mbaya ya kimapenzi

See also:

  1. Njia zinazotumika Kuondoa Harufu Mbaya Ukeni
  2. Zijue Dalili za Upungufu wa Nguvu za Kiume na Tiba Zake
  3. Vyakula vya kuimarisha misuli ya uume
  4. Sababu za kushindwa kusimamisha uume
  5. Jinsi ya kuangalia mechi za Ligi kuu Tanzania kwenye simu (LIVE)
  6. Dawa YA KUMFANYA mpenzi akupende