TETESI ZA USAJILI: Dube anukia Jangwani

TETESI ZA USAJILI 2024

TETESI ZA USAJILI: Dube anukia Jangwani – Inasemekana Klabu ya Yanga inamuhitaji sana mshambuliaji wa Azam FC Prince Dube. Wanaamini Dube anaweza kuwa mbadala sahihi kuchukua nafasi ya Fiston Mayele.

Inaaminika Yanga wamekuwa wakihangaika kumshawishi mchezaji huyo kwa muda mrefu kutua kikosini kutokana na uwezo wake.

Hivi karibuni Azam Fc ilipokuwa mikoani kwa mechi za Ligi Kuu, Dube walionekana kwenye Uwanja wa Mkapa wakishuhudia mechi ya Yanga ambapo walishinda mabao 4-0 dhidi ya Vigogo wa Algeria CR Belouizdad, Dube hakusafiri na Azam kwa sababu ni majeruhi na. amekosa michezo kadhaa mpaka sasa.

Nyota huyo hajacheza mechi ya Azam Fc tangu Februari 19 alipoingia kipindi cha pili dhidi ya Tabora United, hakusafiri na timu katika michezo miwili ya mkoa wa Mbeya dhidi ya Prison na Mwanza dhidi ya Singida.

TETESI ZA USAJILI: Dube anukia Jangwani

TETESI ZA USAJILI: Dube anukia Jangwani

Kwa kanuni ya Azam, mchezaji hata akiwa majeruhi lazima asafiri na timu ili awe sehemu ya kuijenga Umoja. Hata hivyo, Dube hakusafiri, inasemekana alikataa kusafiri kama sehemu ya shinikizo la kuachiliwa.

Habari za ndani ni kwamba kuna mfanyakazi mmoja wa Yanga ambaye awali alikuwa Azam anachora ramani ya Dube kuhamia Jangwani na klabu ina uhakika kuwa suala hilo litakwenda sawa kwani nyota huyo ameanza kuingia kwenye mfumo na mpaka sasa ametuma barua rasmi ya kuvunja mkataba.

See also:

Tarehe ya Droo ya Klabu Bingwa Afrika yatajwa

Nchi zinazotoa wawakilishi wa wili Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025

CAF Rankings 2024 Baada ya Hatua ya Makundi

Majina ya Waliochaguliwa Form Five 2024

Jinsi ya Kubadili Combination Form Five 2024

Ratiba ya Mtihani Form Six 2024 | Kidato cha Sita

Ratiba ya CAF Robo Fainali 2024

Ratiba ya Simba Mwezi March Ligi Kuu NBC 2024

Nauli na bei ya tiketi za treni TRC Tanzania

Jinsi ya Kupiga Kura Mchezaji Bora wa Mwezi Yanga

Matola Kuelekea Mchezo wa Simba vs Tanzania Prisons Kesho

Prince Dube aomba kuondoka Azam

MSIMAMO Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania 2023/2024

Nchi Salama Zaidi za Afrika za Kutembelea 2024