Jinsi ya kupata passport ya kusafiria

Jinsi ya kupata passport ya kusafiria – Kuomba hati ya kusafiria nchini Tanzania ni mchakato muhimu kwa raia wa Tanzania wanaotaka kusafiri nje ya nchi. Katika makala haya, tutakupa taarifa zote muhimu kuhusu jinsi ya kuomba pasipoti nchini Tanzania.

Lakini kabla ya hapo, ni vyema ikumbukwe kwamba Pasipoti ni moja ya hati nyeti sana iliyotolewa na serikali kwa raia wake ili kuwaruhusu kusafiri nje ya nchi kwa madhumuni mbalimbali.

VIELELEZO VINAVYOHITAJIKA WAKATI WA UJAZAJI WA FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI

Cheti cha Kuzaliwa Mwombaji
Cheti/Kiapo cha Kuzaliwa Mzazi wa Mwombaji
Kitambulisho cha Taifa
Picha ya Mwombaji ya hivi karibuni yenye kivuli cha rangi ya buluu isiyokoza (Light blue Background)
Ada ya Fomu Tsh 20,000
Ushahidi wa Safari au Ushahidi wa Shughuli anayofanya Mwombaji.

Jinsi ya kupata passport ya kusafiria

JINSI YA KUJAZA FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI

  1. Bofya Anza kujaza fomu, kwa Ombi Jipya
  2. Bofya ENDELEA ili kuendelea na Ombi ambalo halikufikia mwisho Utahitajika Kujaza Namba ya Utambulisho (Rfeference ID) wa Ombi lako na Namba ya Ombi (Application Number) husika
  3. Jaza Taarifa zako sahihi kwa ukamilifu
  4. Hifadhi Namba yako ya Utambulisho (Application ID) kwa matumizi ya baadaye.
  5. Jaza Taarifa za Pasipoti ya zamani (ikiwa uliwahi kuwa na pasipoti)
  6. Jaza Taarifa za Wadhamini na Watu ambao ungependa wapewe taarifa endapo utatakewa na tatizo lolote
  7. Ambatanisha Vielelezo vyote vinavyohitajika (kwa kuzingatia maelekezo)
  8. Hakiki Taarifa zako zote na kisha bofya kukubaliana nazo ikiwa ziko sahihi
  9. Lipia fomu yako baada ya kupatiwa Namba ya Kumbukumbu ya Malipo (Control Number)
    Kitufe cha Kufuatilia Hali (Status) ya Ombi kinakuwezesha kufuatilia Ombi lako limefikia hatua gani

See also: