Viingilio vya mchezo wa Yanga vs Mamelodi Sundowns Robo Fainali CAFCL

Yanga vs Mamelodi Sundowns

Viingilio vya mchezo wa Yanga vs Mamelodi Sundowns Robo Fainali CAFCL – Viongozi wa Klabu yetu hawana tamaa ya fedha, ndio maana tumepunguza na kuondoa tiketi ya mzunguko kwa lengo la kuhakikisha wengi waje Uwanjani. Tumeweka maslahi ya mpira wa Tanzania mbele. Mechi ya Mamelodi ni kubwa mno lakini kwa kuwa lengo sio fedha ni hamasa basi tunawasihi mashabiki kujitokeza kwa wingi. Kiasi cha fedha ambacho ungelipia tiketi ya mzunguko basi utatumia kama nauli ya usafiri wa kukufikisha uwanjani na baada ya mchezo wetu uweze kurudi nyumbani salama” AliKamwe

“Uongozi wa Klabu umekubaliana kuweka mkakati wa kupeleka mashabiki Afrika Kusini kwenye mchezo wa marudiano. Kama tulivyofanya wakati wa mchezo wetu wa nusu fainali CAFCC dhidi ya Marumo, (kwao kama kwetu) season 2 inaanza na Bei ya kushiriki ni ile ile tshs 2000 tu.

Vile vile tumeaanda usafiri wa kwenda Afrika Kusini kwa njia ya basi, ambapo utahitaji kuwa na kiasi cha Tsh 600,000 gharama za kwenda na kurudi. Watu 10 kutoka Morogoro tayari wameshalipa, endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii tutaweka utaratibu wa namna ya kulipia” amesema AliKamwe

Viingilio vya mchezo wa Yanga vs Mamelodi Sundowns Robo Fainali CAFCL

Viingilio vya mchezo wa Yanga vs Mamelodi Sundowns Robo Fainali CAFCL
Viingilio vya mchezo wa Yanga vs Mamelodi Sundowns Robo Fainali CAFCL

See also: