TAMISEMI YATAKIWA KUTOA ORODHA YA SHULE ZA MRADI WA SEQUIP
TAMISEMI YATAKIWA KUTOA ORODHA YA SHULE ZA MRADI WA SEQUIP – KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imeielekeza Ofisi ya Rais-TAMISEMI kutoa orodha ya Shule za Sekondari zilizokamilika na ambazo hazijakamilika zinazojengwa kupitia mradi wa kuimairisha ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) awamu ya kwanza.
Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe Denis Londo leo wakati wa kikao cha kamati hiyo cha kujadili taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti fungu 77 kwa mwaka 2023/24 kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Februari 2024 na mapendekezo ya mpango wa bajeti kwa mwaka 2024/25 kwa mikoa mitatu ya Mara, Dar es Salaam na Njombe.
Kikao hicho kimefanyika katika kumbi za Bunge jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe
@Ndejembi, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Sospeter Mtwale pamoja na wakuu wa mikoa yote mitatu.
See also:
- Tabora United imeachana na Kocha Goran Copunovic
- Hali ya Wachezaji wa Yanga ambao walipata majeraha
- Viingilio vya mchezo wa Yanga vs Mamelodi Sundowns Robo Fainali CAFCL
- Mada za kuchat na mpenzi wako usiku
- KIKOSI cha Taifa Stars vs Bulgaria Leo 22/03/2024
- MATOKEO Taifa Stars vs Bulgaria Leo 22/03/2024
- A Level Combinations Tanzania
- Zijue Tahasusi (Combination) mpya za kidato cha tano zitakazoanza kutumika Julai
- Hii ni Vita ya Miguel Gamondi na Mamelodi Sundowns
- Viingilio vya mechi ya Simba dhidi ya Al Ahly 29/03/2024
Leave a Reply