Al Hilal ya Sudan kucheza Ligi Kuu Tanzania – Klabu ya AL Hilal ya Sudan imetuma maombi kwa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, ya kucheza Ligi Kuu ya Tanzania kuanzia msimu ujao.
Afisa habari wa TFF, Clifford Ndimbo amezungumza na Jamhuri Media na kulifafanua suala hilo.
“Ni kweli wameomba na tumewakubalia, lakini watakuwa wanacheza kama mechi za kirafiki, matokeo yao hayatajumuishwa lakini watakuwepo kwenye ratiba, lengo ni kuwasaidia wakati huu ambao wapo kwenye majanga lakini pia itaongeza Ligi kufuatiliwa zaidi.
“Itasaidia kuongeza ushindani kwa Klabu kucheza na timu kama Al Hilal ambayo sio rahisi kuipata kucheza nayo, mbali na timu, waamuzi wao pia watakuwa sehemu ya waamuzi wa ligi yetu” amesema Ndimbo
Al Hilal inayonolewa na kocha Florent Ibenge kwa sasa wapo kileleni mwa ligi kuu ya Sudan wakiwa na pointi 53, huku wakiwa na nyota kama Issa Fofana na Mohamed Abdulrahman.
See also:
- Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Leo
- Klabu ya Al Hilal kucheza Ligi Kuu ya NBC Tanzania
- Gharama za kupata passport Tanzania
- Jinsi ya kupata passport ya kusafiria
- Jinsi ya Kuomba Pasipoti nchini Tanzania 2024
- Vifurushi vya Azam TV vya wiki na siku
- Jinsi ya Kuomba Pasipoti nchini Tanzania 2024
- Ratiba ya Ligi Kuu England 2023/24 EPL
- Idadi Ya Makombe Ya Man City
- UEFA Champions League: Ratiba na Droo ya Robo & Nusu Fainali
Leave a Reply