Alikiba Azindua CROWN TV Itaonekana Kupitia Azam TV

Alikiba Azindua CROWN TV Itaonekana Kupitia Azam TV — Mashabiki Wajadiliana Kati ya Wasafi na Crown TV

Leo, staa wa Bongo Fleva Alikiba amezindua rasmi kituo chake cha televisheni, CROWN TV, ambacho kitakuwa hewani kupitia kisimbuzi cha Azam TV, kwenye chaneli namba 415. Kwa kauli mbiu ya “Burudani Kwa Wote,” CROWN TV ina lengo la kuleta burudani na vipindi vya kipekee kwa watazamaji wake.

Uzinduzi huu umekuja kama hatua nyingine muhimu kwa Alikiba katika kupanua ushawishi wake siyo tu kwenye muziki, bali pia kwenye sekta ya burudani kwa ujumla. CROWN TV inatarajiwa kushindana moja kwa moja na kituo kingine maarufu, Wasafi TV, kinachomilikiwa na Diamond Platnumz, mpinzani wake mkuu kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Alikiba Azindua CROWN TV Itaonekana Kupitia Azam TV
Alikiba Azindua CROWN TV Itaonekana Kupitia Azam TV

Mashabiki wa burudani na muziki sasa wanajikuta wakijiuliza ni wapi watapata burudani bora zaidi kati ya CROWN TV na Wasafi TV. Uzoefu wa Alikiba na timu yake unategemewa kutoa maudhui yanayovutia na tofauti, huku mashabiki wakiwa na fursa ya kuchagua kituo cha kutazama kulingana na ladha zao za burudani/Alikiba Azindua CROWN TV Itaonekana Kupitia Azam TV.

Wewe utachagua wapi? Kule Wasafi TV au hapa CROWN TV?

ANGALIA PIA: