Arsenal Imepata Ushindi dhidi ya Spurs kwenye London Dabi

Arsenal Imepata Ushindi dhidi ya Spurs kwenye London Dabi | Arsenal Yaibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo EPL dhidi ya Tottenham Hotspurs ikiwa ni Derby ya London.

Arsenal Imepata Ushindi dhidi ya Spurs kwenye London Dabi

Baada ya miaka 36 kupita sasa Arsenal anafanikiwa kushinda michezo mitatu mfululizo ya Dabi ya London dhidi ya Spurs baada ya ushindi wa leo wa goli 1-0 kwenye uwanja wa Spurs.

Mchezo wa leo umetoa taswira tofauti na michezo iliyopita ya Dabi ya London ambapo ilimalizika kwa timu zote kupata goli na ikishuhudia mechi kuwa na magoli mengi. Itakumbukwa msimu ulioisha walipo kutana kwenye michezo miwili ya ligi kuu Arsenal alifanikiwa kufunga goli 5 wakati Spurs akifunga goli 3.

Goli la ushindi limefungwa na beki kitasa wa Arsena Gabliel kwa kichwa cha kuonganisha baada ya kona kupigwa na Saka dakika ya 64 ya mchezo. Hii inadhihirisha uhatari wao kwenye mipira ya kutenga maana kabla ya hapo walisha funga magoli 22 kwa mwaka huu kwa mipira ya kutenga na ndio timu inayoongoza kwa kufunga kwenye mipira ya kutenga.

Arsenal Imepata Ushindi dhidi ya Spurs kwenye London Dabi
Arsenal Imepata Ushindi dhidi ya Spurs kwenye London Dabi

Baada ya mchezo huu kutamatika sasa Arsenal anakwenda kujianda dhidi ya michezo migumu mingine iliyopo mbele yake kama vilie mchezo dhidi ya Atalanta (Chamipons League) tarehe 19 Septembe na Manchester City (Ligi Kuu EPL) tarehe 22 september.

Rasmi sasa Arsenal anapaa kwenye msimamo wa Ligi Kuu EPL mpaka nafasi ya pili chini ya Man City kwa alama 10 akiwa amefunga goli 6 na kuruhusu goli 1 kwenye michezo 4 ya ligi waliocheza/Arsenal Imepata Ushindi dhidi ya Spurs kwenye London Dabi.

TOA MAONI YAKO! Umekionaje kiwango cha Arsenal msimu huu na Je! matumaini yakuchukua ubingwa kwao bado yapo?

ANGALIA PIA: