Azam yatangaza kuachana na Dube RASMI

Azam yatangaza kuachana na Dube RASMI | KLABU ya Azam FC imeridhia kuondoka kwa mshambuliaji wake Mzimbabwe, Prince Mpumelelo Dube (27) kufuatia kukamilisha taratibu za kuvunja mkataba wake.

Dube alijiunga na Azam FC Agosti mwaka 2020 akitokea The Highlanders ya kwao, Bulawayo baada ya awali kuzitumikia SuperSport United na Black Leopards kwa vipindi tofauti.

Azam yatangaza kuachana na Dube RASMI

Azam yatangaza kuachana na Dube RASMI
Azam yatangaza kuachana na Dube RASMI

TAARIFA

Tunapenda kuutarifu umma kwamba tumeridhia maombi ya Prince Dube kuvunja mkataba wake nasi, aliyoyatoa Machi 2024.

Hatua hii inafuatia kitendo cha mchezaji huyo kutimiza matakwa ya kimkataba kama ilivyoainishwa kwenye vipengele vinavyoruhusu upande mmoja kuvunja mkataba.

Tunamtakia kila la kheri katika safari yake ya soka na maisha kwa ujumla.

Imetolewa na Menejimenti, Azam Football Club, Juni 28, 2024.

SEE ALSO: