Bei ya Leseni ya Biashara Tanzania 2024

Leseni ya Biashara Tanzania

Bei ya Leseni ya Biashara Tanzania 2024 | Leseni zote za Biashara hutolewa chini ya Sheria ya Biashara Na. 25 ya mwaka 1972 na marekebisho yake yaliyofanyika mwaka 2014.

Mwombaji wa Leseni ya biashara anapaswa ajaze fomu ya maombi ya leseni TFN 211 (Business license application form).

MALIPO:

Serikali ilirudisha rasmi utoaji wa ada za Leseni za biashara kupitia Sheria ya Fedha Na. 5 ya mwaka 2011. Kutokana na marekebisho hayo, utaratibu wa kutoa Leseni za biashara bila malipo uliondolewa na kurudishwa ada ya Leseni kuanzia 30 Juni, 2013.

Kutokana na marekebisho hayo, utaratibu wa kutoa Leseni za biashara bila malipo uliondolewa na kurudishwa ada ya Leseni kuanzia 30 Juni, 2013.

Kiwango cha ada ya Leseni kinatofautiana kulingana na aina ya biashara husika na eneo ilipo biashara hiyo. Mfano : kiwango cha ada za Leseni kwa Halmashauri ya Jiji na Manispaa ni tofauti na za Halmashauri ya Wilaya na maeneo ya Vijijini. Baada ya ulipaji wa ada hiyo mfanyabiashara atapatiwa stakabadhi kwa malipo halali ya Fedha yake.

Bei ya Leseni ya Biashara Tanzania 2024

See also