UTT AMIS 2024
Bei ya vipande vya UTT AMIS 2024 | UTT AMIS ni taasisi ya Serikali ya Tanzania iliyo chini ya Wizara ya Fedha ambayo dhumuni lake kuu ni kuanzisha na kuendesha mifuko ya uwekezaji wa pamoja hapa nchini ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kujiwekea akiba na kuwekeza katika masoko ya fedha na mitaji.
Bei ya vipande vya UTT AMIS 2024: Changamoto kubwa iliyopo ni kwamba bado hali ya utamaduni wa kuweka akiba na kuwekeza katika masoko ya fedha na mitaji bado iko chini kwa sababu za kihistoria, kijamii, kiuchumi na wakati mwingine sababu huwa ni kipato kidogo na mahitaji ni mengi. Ukweli unabaki ya kuwa hakuna siku fedha zinaweza kutosha.
Hivyo inamlazimu kujenga nidhamu na tabia ya kujiwekea akiba ya fedha kutokana na kipato anachapata. Siyo jambo rahisi kuweza kuweka akiba ya fedha, lakini ili uweze kufanya hivyo ni muhimu kujenga nidhamu katika matumizi yetu.
Afisa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Rahim Mwanga anasema “Suala si kuweka akiba na kuwekeza tuu, ila tunatakiwa kuweka akiba na kuwekeza kwa ufanisi ambao ni Uwekezaji unaozingatia kuwa na malengo, kuweka mpango wa kufikia malengo na muda. Mfano lengo ni kuwa na milioni 5, kwa muda wa miaka 3 na utawekeza kila mwezi. Hiyo ndiyo itakayo kuwa dira ya kukuwezesha kufika malengo.
Bei ya vipande vya UTT AMIS 2024: Afisa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Rahim Mwanga anasema, “Siku zote ukiwa na akiba ya fedha unatakiwa kuziwekeza. Uwekezaji ni dhana pana, kwa mfano, mwingine anataka kununua kiwanja, mwingine aanzishe biashara, mwingine ampeleke mtoto shule, mwingine akasome yeye mwenyewe, lengo likiwa ni kwamba ile fedha ya akiba ilete matokeo chanya kwake. Hata hivyo, inatakiwa ieleweke kwamba kuna muda kati ya kuweka akiba, kuwekeza na kutimiza lengo.
Bei ya vipande vya UTT AMIS 2024
- Net Asset Value Per Unit (Tsh) – 995.0318
- Sale Price Per Unit (Tsh) – 995.0318
- Repurchase Price Per Unit (Tsh) – 985.0814
Kwa mfano, ninataka kuweka akiba kwa ajili ya elimu ya mwanangu ambaye ana mwaka mmoja sasa, kwa hiyo kuna miaka miwili au mitatu baadaye aanze chekechea, kwa hiyo nikiweka akiba tu katika sehemu ambayo haikuwi katika miaka mitatu hiyo maana yake itakuwa haina tija kwa sababu hapo katikati lazima kutakuwa na mfumuko wa bei na mambo mengine, kwa hiyo kinachotakiwa ni kuwekeza fedha hizo za akiba kabla ya kuja kufanya uwekezaji wa kumpeleka mtoto shule.
Kwa hiyo hapa katikati niwekeze wapi sehemu ambayo ipo salama au itanipa tija nzuri na haitanihitaji kuhangaika sana. Sasa sehemu hizi watu wengi hawajazichangamkia. Sehemu hizo ni katika masoko ya fedha na masoko ya mitaji.” Anasema, “Tunapozungumzia masoko ya mitaji mfano wake ni Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), kwani katika soko hili kuna makampuni yamejiorodhesha yakiuza mitaji na kutafuta mitaji kwa kuuza hisa, kwa hiyo ni sehemu mojawapo ambayo watu wanaweza kwenda kuwekeza pia katika dhamana za serikali za muda mrefu.
Bei ya vipande vya UTT AMIS 2024: Dhamana za kapuni(Corporate bonds) na katika Vipande. Sehemu nyingine ni katika masoko ya fedha huku kuna akaunti za muda maalumu (fixed deposit accounts) na akaunti ambazo hazina muda maalumu (call deposit accounts), pia kuna dhamana za Serikali.
Bei ya vipande vya UTT AMIS 2024: Mwekezaji anaweza kuwekeza moja kwa moja katika dhamana hizo hapo juu, lakini kuna changamoto za mwekezaji mmoja mmoja kufikia soko na kunufaika kikamilifu, kama vile elimu ya kutosha, urahisi wa kuwekeza na kutoka na faida nzuri.
Lakini kupitia UTT AMIS changamoto hizo zinapungua kupitia kuwekeza kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja. Mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni fursa inayomuwezesha mtu mmoja mmoja au taasisi, kampuni kuwekeza rasilimali fedha zao kupitia UTT AMIS(Meneja) na UTT AMIS kazi yetu ni kuwekeza kwa niaba yao yaani mtu mmoja mmoja, taasisi au makampuni katika dhamana hizo kulingana na sera ya Uwekezaji ya mfuko.”
Anasema, ” Umiliki wa Uwekezaji katika katika mfuko wa uwekezaji wa pamoja huitwa kipande (unit). Miongoni ya faida kubwa ambayo mwekezaji anaipata kwa kujiunga na mifuko ya uwekezaji wa pamoja badala ya kuwekeza mmoja mmoja katika masoko ya fedha na masoko ya mitaji ni faida shindani ukilinganisha na baadhi ya bidhaa za aina hiyo sokoni.”
Mwanga anasema, “Kwa mfano, katika benki tukitumia akaunti ya muda maalumu (fixed deposit accounts), katika akaunti hii benki inamlipa mwekekezaji anayewekeza katika akaunti hiyo kulingana na muda na kiasi anachowekeza na kiwango cha chini cha kuwekeza katika benki ni milioni moja au laki tano.
ANGALIA PIA:
- Jinsi ya kulipia Vifurushi vya StarTimes kwa siku
- Jinsi ya kujiunga na vifurushi vya Startimes
- Bei ya Vifurushi vya Startimes kwa Wiki
- Bei ya Vifurushi vya Startimes 2024
- Jinsi ya kubadilisha kifurushi cha Azam TV
- Bei ya Vifurushi vya Azam TV vya Wiki
- Bei ya Vifurushi vya Azam Antena
- Bei ya Vifurushi vya Azam TV 2024
- Bei ya Leseni ya Biashara Tanzania 2024
- Bei Mpya ya Mafuta Petroli, Dizeli na Mafuta ya taa
- Bei ya Madini ya Almasi Tanzania
- Bei ya Madini ya Tanzanite Tanzania 2024
- Bei ya Madini ya Silver Tanzania 2024
Leave a Reply