Dawa YA KUMFANYA mpenzi akupende

Dawa YA KUMFANYA mpenzi akupende: Baadhi ya watu wamekua wakijiuliza ni jinsi gani wanaweza wafanya wapenzi wao wawawaze kila mara au mara kwa mara. Kuna muda wazo hili humjia mtu baada ya kuona anapuuzwa kiasi flani na mpenzi wake au akiwa na hitaji la kumuweka mpenzi wake karibu zaidi.

Kama ni moja kati ya watu ambao wanataka kujua juu ya hili kwasababu hiyo au sababu nyingine tofauti. The bestgalaxy inakupa mwanga kidogo juu ya hili hapa chini. Tunaenda kuangalia vitu vichache unavyoweza jaribu kumfanya mpenzi wako akuwaze mara kwa mara.

Dawa YA KUMFANYA mpenzi akupende

Uwe msaada na mshauri wake mzuri

Mukiwa kwenye mahusiano mpenzi wako anaweza kuwa na matatizo ambayo huitaji umshauli au umsaidie kwanjia nyingine. Endapo utakua msaada na mshauri mzuri kwake basi utakua kichwani mwake kila mara maana tukiwa kama binadamu hua mara nyingi tunahitaji msaada.

Hakikisha haupuuzi matatizo yake na hata yakikushinda fanya kumshauri kwa maneno mazuri. Na usiwe msaada kwenye matatizo tu, hata kwenye nyakati za furaha kuwa nae. Kusaidia kunaweza jumuisha kumpa pesa maana vitu vingi kwenye maisha ya sasa huitaji pesa .

Uwe unampa ahadi

Katika mahusiano ahadi zinaweza fanya hata mahusiano yadumu maana mnakua mnajua mnakoelekea. Ni vema sana ukawa unampa ahadi mpenzi wako na ahadi hizi zinaweza kuwa kubwa au ndogo lakini tambua kuwa ahadi ni deni kwa mpenzi wako. Unaweza huahidi mpenzi wako kuhusu vitu vya kesho, mwezi ujao, mwakani na hata maishani. Mtu anaekudai atakua anakukumbuka hata ukisahau wewe.

Dawa YA KUMFANYA mpenzi akupende

Ila tambua tu ahadi ni deni na kuna baadhi ya ahadi huharibu mpaka maisha ya mtu. Mfano; unamuahidi mtu mtaoana alafu anazama kwenye penzi na kukupa moyo wote mpaka maisha alafu unaanza kumuona mjinga kisa akili yote ipo kwako na hutaki muoane tena. Ivi nafikili maisha yake utakua umeyavuruga kiasi gani?. Unaweza kuwa umewahi pewa ahadi kubwa za uongo lakini jambo hilo likufuze kuwa mkweli na sio muongo.

Ukiwa nae hakikisha mnakua na furaha

Kuna nyakati nyingine kwenye mahusiano mnaweza kuwa na hasira au maugovi lakini nyakati ambazo hata mkiachana au mkiwa mbali mnaziwaza ni nyakati zile za furaha. Ukiwa kwenye mahusianao hakikisha ukiwa na mpenzi wako unakua chanzo cha furaha na sio maugomvi. Mpenzi wako anaweza kua amekufanya uchukie lakini pamoja na kuchukia kwako hakikisha unamaliza utata na unatengeneza hali ya furaha ukiwa nae maana nyakati za furaha ndio nyakati ambazo tunaziwaza sana.

Mfano; Kuna muda unaweza chati na mpenzi wako vizuri mpaka ukarudia kusoma sms mara kumi kwa siku huku ukimuwaza. Au umeongea nae vizuri muda uliopita lakini tukio zima la maongezi yenu lipokichwani unaliwaza kila mara huku ukitabasamu. Hii inaweza kuwa ni kwasababu mulikua kwenye nyakati inayofurahisha na Kama tunavyofahamu, hakuna mtu asiependa kuziwaza nyakati zinazofurahisha.

Pia usisahau kutumia maneno ya upendo na kumsifu ili ajisikie vizuri na kupata furaha. Pambana kutengeneza nyakati za furaha mkiwa wote alafu hizi nyakati zitatengeneza historia nzuri ya mahusiano yenu ambayo mtakua mkivutiwa kuendelea kuiandika.

See also:

  1. Ijue Sayansi ya Ute ukeni, Rangi, harufu na mazingatio yake
  2. Faida za Kiafya za Kufanya Mapenzi Salama
  3. Namna ya kuchati na mpenzi wako
  4. Mambo ya kuzingatia kabla ya kununua bidhaa Mtandaoni (Online)
  5. Vifurushi vya Tigo Na bei zake
  6. Kamene Secondary School fees, location, photos