Dirisha la Masahihisho Maombi ya Mikopo HESLB 2024/2025 Lafunguliwa

Dirisha la Masahihisho Maombi ya Mikopo HESLB 2024/2025 Lafunguliwa | Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Yatoa Muda wa Masahihisho kwa Waombaji wa Mwaka 2024/2025

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imewataarifu waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2024/2025 kuwa baadhi ya maombi yao yanahitaji marekebisho. Baada ya kufanya uhakiki wa awali, imebainika kuwa maombi hayo yanahitaji kufanyiwa masahihisho kabla ya hatua za mwisho za uhakiki.

Dirisha la Masahihisho Maombi ya Mikopo HESLB 2024/2025 Lafunguliwa

Dirisha la kufanya marekebisho haya litafunguliwa kwa muda wa siku 7, kuanzia tarehe 15 hadi 21 Septemba 2024. Katika kipindi hiki, waombaji wote wanaopaswa kufanya marekebisho watahitajika kuingia kwenye akaunti zao walizotumia wakati wa kuomba ili kufanya masahihisho husika.

Aidha, Bodi ya Mikopo imesisitiza kuwa maombi mapya hayatapokelewa katika kipindi hiki, kwani dirisha la maombi limefungwa rasmi tarehe 14 Septemba 2024. Waombaji wanashauriwa kuchukua hatua stahiki ndani ya muda uliopangwa ili kuhakikisha maombi yao yanaendelea kushughulikiwa.

Hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anapata fursa ya kupata mkopo unaohitajika kwa ajili ya masomo yake, ikiwa maombi yamekamilishwa ipasavyo/Dirisha la Masahihisho Maombi ya Mikopo HESLB 2024/2025 Lafunguliwa.

ANGALIA PIA: