Fomu ya Kuomba Mkopo HESLB 2024/2025

Fomu ya Kuomba Mkopo HESLB 2024/2025 Higher Education Students’ Loans Board | Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwafahamisha Waombaji wa mikopo na Umma kwa ujumla kuwa muda wa kuwasilisha maombi ya mikopo umeongezwa mbele hadi tarehe 14 Septemba, 2024.

Hatua hii imechukuliwa ili kuwapa fursa wale ambao kwa sababu mbalimbali hawakuweza kufanya maombi ya mikopo katika muda uliokuwa umepangwa.

Itakumbukwa kuwa, awali Bodi ilianza kupokea maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao tarehe 1 Juni, 2024 na mwisho wa kuwasilisha maombi ulipangwa kuwa tarehe 31 Agosti, 2024/Fomu ya Kuomba Mkopo HESLB 2024/2025.

Kupitia tangazo hili, waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2024/2025 ambao hawajakamilisha maombi yao wanashauriwa kukamilisha na kuwasilisha maombi yao ya mikopo ndani ya muda ulioongezwa.

Bodi inapenda kusisitiza kuwa hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada ya tarehe 14 Septemba, 2024.

Fomu ya Kuomba Mkopo HESLB 2024/2025

Dkt. Kiwia aliwakumbusha wanahabari kuhusu miongozo mitano ya utoaji mikopo iliyozinduliwa Mei 27, 2024 na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Prof. Adolf Mkenda (Mb), kuwa ni pamoja na;

Fomu ya Kuomba Mkopo HESLB 2024/2025
Fomu ya Kuomba Mkopo HESLB 2024/2025

i. Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Shahada ya Awali (Bachelor) kwa 2024 -2025,

ii. Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Stashahada (Diploma) kwa 2024 – 2025,

iii. Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Stashahada ya Umahiri katika Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo  kwa 2024 – 2025 (Post Graduate Diploma in Legal Practice),

iv. Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Shahada za Umahiri na Uzamivu, na

v. Mwongozo wa Utoaji Ruzuku za Samia kwa mwaka 2024 – 2025

Katika mwaka wa fedha wa 2024/2025, serikali imetenga TZS 787 bilioni kwa ajili ya mikopo na ruzuku kwa jumla ya wanafunzi 250,000. Idadi hii ya wanafunzi imeongezeka kutoka wanafunzi 224,056 mwaka 2023/2024. Hivyo, kwa mwaka ujao wa masomo kutakuwa na ongezeko la jumla ya wanafunzi 25,944.

ANGALIA PIA: