Harry Kane Aandika Historia Mpya UEFA, Avunja Rekodi ya Rooney

Harry Kane Aandika Historia Mpya UEFA, Avunja Rekodi ya Rooney | Harry Kane Aandika Historia Mpya: Avunja Rekodi ya Wayne Rooney Katika Ligi ya Mabingwa

Harry Kane ameendelea kuweka historia ya kipekee baada ya kufunga mabao manne kwenye ushindi wa Bayern Munich dhidi ya Dinamo Zagreb katika Ligi ya Mabingwa UEFA. Nahodha huyo wa Uingereza alifunga penalti dakika ya 19, na kwa bao hilo, Kane alifikisha mabao 50 katika mashindano yote akiwa na Bayern Munich.

Kwa bao hilo, Kane alifikisha mabao 30 katika Ligi ya Mabingwa, akilingana na rekodi ya Wayne Rooney kwa wachezaji wa Uingereza. Hata hivyo, kipindi cha pili Kane aliipita rekodi hiyo kwa kuifungia Bayern mabao matatu zaidi, kufikisha jumla ya mabao manne katika mechi hiyo, na kuandika historia mpya kwa kufunga mabao 33 katika michuano hiyo mikubwa ya Ulaya.

Harry Kane Aandika Historia Mpya UEFA, Avunja Rekodi ya Rooney
Harry Kane Aandika Historia Mpya UEFA, Avunja Rekodi ya Rooney

Kane ameifungia Bayern Munich mabao 12 kati ya hayo 33, huku mabao 21 yakiwa wakati alipokuwa na Tottenham Hotspur. Rekodi yake ya Ligi ya Mabingwa ilianza mwaka 2016, alipofunga bao lake la kwanza dhidi ya AS Monaco.

ANGALIA PIA: