Jinsi ya kujiunga na JKT 2024/2025

JKT 2024/2025

Jinsi ya kujiunga na JKT 2024/2025 | Jeshi la kujenga Taifa(JKT) limekuwa linapokea na kuendesha Mafunzo yahusuyo Ulinzi wa Taifa, uzalendo, Ujasiliamali, Ujasili (kupitia mafunzo ya Kilimo, Ufugaji na Biashara) kwa nyakati tofauti tofauti kadri ya maelekezo kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Vijana wa Kujitolea:

Hawa ni vijana wa JKT wanaojiunga na JKT kwa mkataba wa hiari kwa muda usiopungua miaka miwili (2). Mara baada ya kuandikishwa, vijana hao hupelekwa katika kambi mbalimbali za JKT kwa ajili ya kupata elimu na mafunzo.

Vijana wa Utekelezaji wa Sheria:

Hawa ndio vijana wanaojiunga na JKT kwa mujibu wa sheria. Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanatumikia JKT kwa muda usiopungua miezi (3). Hivi sasa vijana wanaohusika na sheria hiyo ni wale wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kutoka shule mbalimbali za Tanzania Bara.

Jinsi ya kujiunga na JKT 2024/2025

JKT huajiri vijana wa kujitolea kutoka mikoa yote nchini kila mwaka. Utaratibu uliotumika ni JKT kuwaandikia barua wakuu wa Mikoa na kuoanisha nafasi ambazo mkoa umepewa.

Baada ya Mkoa kupokea barua kutoka kwa Mkuu wa JKT yenye idadi ya nafasi za vijana waliopangwa kujiunga. Mkoa unasambaza nafasi hizo kulingana na wilaya zake. Wilaya pia zinatakiwa kupeleka tarafa, kata na vijiji. Mara nyingi uongozi wa wilaya huweka tangazo la nafasi hizo kwenye ubao wao wa matangazo.

JKT inatangaza nafasi za kujiunga na jeshi hilo kupitia vyombo vya habari vya Serikali na binafsi kwa nia ya kuharakisha taarifa hizo. kia wananchi hasa vijana. Usaili wa awali unafanyika chini ya Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya wanazotoka vijana hao, baadaye hufanyika mkoani humo, ili kupata idadi ya vijana katika mkoa mzima.

Zoezi hilo likikamilika mikoani, JKT hutuma timu za maofisa na askari kutoka Makao Makuu ya JKT kuwakagua vijana waliohojiwa katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Vijana wanapimwa afya zao na kusafirishwa hadi vikosi vya JKT.

Jinsi ya kujiunga na JKT 2024/2025

Masharti kwa vijana wa kujitolea kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa.

1. Awe raia wa Tanzania
2. Awe na umri kati ya miaka 18-23
3. Awe amemaliza darasa la saba na kuendelea
4. Asiwe ameolewa au kuolewa na asiwe na mtu anayemtegemea
5. Awe tayari kufuata sheria zote za kijeshi zitakazotumika kwake akiwa jeshini (kutoroka, wizi, ulevi, kuvuta bangi, madawa ya kulevya na kupata mimba n.k) Jeshini ni kosa kubwa. na utaweza kushtakiwa na kufutwa mkataba wako na JKT
6. Awe tayari kurejea nyumbani baada ya kumaliza mkataba wake na Jeshi la Kujenga Taifa
7. Kuwa na tabia na mwenendo mzuri

Mahitaji ya kijana halali kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa.

1. Awe raia wa Tanzania
2. Umri kati ya miaka 18-35
3. Awe amemaliza kidato cha sita na kuendelea
4. Awe tayari kufuata sheria zote za kijeshi zitakazotumika kwake akiwa jeshini (Sigara, dawa za kulevya na mimba atachukuliwa hatua na kufutwa mkataba wake na JKT.
5. Utoro haukubaliki na mkataba utasogezwa mbele endapo utakosekana
6. Kuwa na tabia na mwenendo mzuri

See also:

Jinsi ya kupata namba ya NIDA kwa haraka