Justin Shonga afariki baada ya kuumwa, RIP Shonga

Justin Shonga afariki baada ya kuumwa, RIP Shonga | tunasikitika sana kusikia kuhusu kifo cha Justin Shonga baada ya kuugua kwa muda mfupi. ⛔️

Shonga alikuwa mchezaji wa kipekee na mwenye kipaji kikubwa. Katika maisha yake ya soka, aliwahi kuzichezea klabu kadhaa zikiwemo Nkwazi, Orlando Pirates, TTM, Cape Town City, Ismaily SC, Sekhukhune United, na Najran.

Alikuwa na mchango mkubwa katika Timu ya Taifa ya Zambia, ambapo alicheza mechi 33 na kufunga mabao 16. Mafanikio haya ni ushahidi wa uwezo wake na juhudi zake kubwa katika uwanja wa soka.

Justin Shonga afariki baada ya kuumwa, RIP Shonga
Justin Shonga afariki baada ya kuumwa, RIP Shonga

Kifo chake ni pigo kubwa kwa ulimwengu wa soka, wapenzi wa michezo, na familia yake. Tutamkumbuka daima kwa mchango wake mkubwa na ucheshi wake uwanjani.

Team KIJIWEFORUM tunakuombea Pumzika kwa amani, Shonga! ️

SEE ALSO: