Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Leo

Taifa Stars Squad

Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Leo – FIFA Series ni michuano mipya ya kirafiki ya mwaliko inayoandaliwa na FIFA ikishirikisha timu za taifa zitakazocheza mechi za kirafiki dhidi ya timu kutoka mabara tofauti, na itafanyika mwezi Machi kila mwaka ambayo inagawanywa kwa namba mbili (sufwa). Mwezi huu wa 2024 unafanyika kwa mara ya kwanza.

Michuano hiyo itazikutanisha timu za taifa za wanaume katika mfululizo wa michuano midogo midogo inayoshirikisha timu kutoka mashirikisho sita ya soka ya mabara yanayosimamiwa na FIFA. Kila kundi litakuwa na timu nne na michuano hiyo itafanyika katika kituo kimoja kwa kutumia muda wa mapumziko wa ligi kwa mechi za kimataifa.

FIFA itatoa msaada wa kifedha kwa timu zinazoshiriki michuano hiyo na pia ina jukumu la kuyaandaa kwa ushirikiano na nchi waandaji na vyama wanachama.

NAHODHA wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta ameachwa kwenye kikosi hicho kitakachokwenda Azerbaijan kushiriki michezo ya Fifa Series 2024.

Samatta anayeichezea PAOK ya Ugiriki, alikuwa miongoni wa wachezaji wa kikosi hicho kilichoshiriki fainali za Afcon zilizochezwa kati ya Januari na Februari, mwaka huu nchini Ivory Coast ambako Stars iliishia hatua ya makundi.

Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Leo

Kikosi cha wachezaji 23 kilichoitwa leo na Kaimu Kocha Mkuu, Hemed Suleiman ‘Morocco’/Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Leo:-

Makipa

Aishi Manula (Simba),
Aboutwaleeb Mshery (Yanga),
Kwesi Kawawa (Syrianka FC, Sweden)

Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Leo
Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Leo

Mabeki

Bakari Mwamnyeto,
Ibrahim Hamad ‘Bacca’ (Yanga),
Mohammed Hussein
Kennedy Juma (Simba),
Novatus Dismas (Shakhtar Donestsk, Ukraine),
Miano Danillo (Villena, Hispania)
Haji Mnoga (Aldershot Town, England)

Viungo

Feisal Salum
Yahya Zayd (Azam FC),
Mudathir Yahya (Yanga),
Morice Michael (RFK Novi Sad, Serbia),
Himid Mao (Tala’ea El Gaish SC, Misri)
Tarryn Allarakhia (Wealdstone, England).

Washambuliaji

Clement Mzize (Yanga),
Saimon Msuva (Al najmah FC, Saudia),
Kibu Denis (Simba),
Abdul Suleiman (Azam FC),
Ben Starkie (Likeston Town, England)
Charles M’mombwa (Macarthur FC, Australia).

See also: