Kinara wa Magoli Ligi Kuu Tanzania Bara, Mwalimu Hashikiki

Kinara wa Magoli Ligi Kuu Tanzania Bara, Mwalimu Hashikiki — Msimu huu umechangamka mapema kwenye mbio za ubingwa kulingana na washambuliaji kuwa na uchu na hasiri ya kufunga magoli kila mchezo. Ni mzunguko wa 8 tu ila mpaka sasa baadhi ya washambuliaji wanaonekana kuwa na kiwango bora sana ikiwemo Seleman Mwalimu.

Salum Mwalimu, mshambuliaji wa timu ya Fountain Gate FC na nyota wa Taifa Stars, anaendelea kung’ara katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu. Akiwa tayari amepachika bao lake la sita, amejikita rasmi kuwa kinara wa mabao katika ligi hiyo. Kasi yake ya kufumania nyavu inawavutia mashabiki na wapinzani, na kumweka katika nafasi nzuri ya kutwaa kiatu cha dhahabu msimu huu.

Salum Mwalimu sio tu mshambuliaji tegemeo wa klabu yake, lakini pia ni sehemu muhimu ya kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Uwezo wake wa kufunga mabao kwa muda mfupi umempa sifa kubwa, akiwakilisha Tanzania kimataifa na kuzidi kuimarisha jina lake katika soka la Afrika Mashariki.

Kinara wa Magoli Ligi Kuu Tanzania Bara, Mwalimu Hashikiki

Vinara wa magoli mpaka kufikia mzunguko wa nane wa Ligi Kuu NBC Tanzania Bara msimu huu 2024/2025:-

Kinara wa Magoli Ligi Kuu Tanzania Bara, Mwalimu Hashikiki
Kinara wa Magoli Ligi Kuu Tanzania Bara, Mwalimu Hashikiki

Selemani Mwalimu (Fountain Gate FC) — 6 Goli
Williamu Edgar (Fountain Gate FC) — 4 Goli
Maxi Nzingeli (Yanga SC) — 3 Goli
Elvis Rupia (Singida Black Stars) — 3 Goli
Paul Peter (Dodoma Jiji) — 3 Goli

Je, ataendelea kudumisha kiwango chake bora na kuwa mwokozi wa mabao kwa Fountain Gate FC na Taifa Stars msimu huu? Ni jambo la kusubiriwa kwa hamu.

ANGALIA PIA: