Kocha wa KenGold Fikirini Bakari Afikiria Kujiuzulu Baada ya Kichapo Dhidi ya KMC | Mara baada ya timu yake, KenGold FC, kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya KMC FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, kocha Fikirini Bakari ameweka wazi kuwa anafikiria kujiuzulu nafasi yake kama kocha mkuu.
Fikirini alieleza kuwa ameshindwa kufikia malengo aliyokuwa amepanga na timu hiyo, na sasa ni wakati wa kujitathmini na kuona kama hatua bora ni kuachia nafasi hiyo kwa mtu mwingine.
Kocha Fikirini aliongeza kuwa, licha ya jitihada zake kujaribu kubadilisha mwenendo wa timu, matokeo yamekuwa si mazuri kama alivyotarajia. Kwa hiyo, kama sehemu ya uwajibikaji na heshima kwa timu, anaona busara kufikiria kujiuzulu ili kumpisha kocha mwingine kuendeleza jitihada za timu.
Hali hii inafuatia mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha kwa KenGold FC, ambao kwa sasa wanakabiliwa na presha ya kuboresha nafasi yao katika ligi.
Kocha wa KenGold Fikirini Bakari Afikiria Kujiuzulu Baada ya Kichapo Dhidi ya KMC
“Hadi sasa nipo nje ya malengo, mimi kama mwalimu napaswa kujitathimini, nafikiria bora nikae pembeni nijitathimini na hii inaweza ikawa ndio mechi yangu ya mwisho.”- Fikiri Elias Head Coach KenGold FC.
ANGALIA PIA:
- Wachezaji wanaowania Ballon d’Or 2024 Power Rankings
- Haaland Amefunga Mabao Mangapi Katika Maisha Yake ya Soka?
- Orodha ya Wafungaji Bora MLS 2024/2025 Ligi Kuu USA
- Viingilio Mchezo wa Simba vs Al Ahly Tripoli CAF
- Rekodi za Simba Kwenye Michezo ya Kufuzu Makundi, wakiwa kwa Mkapa
- Matokeo Kagera Sugar vs JKT Tanzania 16/09/2024
- Matokeo KMC vs Kengold Leo 16/09/2024
Leave a Reply