Kozi za Afya: Udaktari
Kozi za Afya: Sifa za kusomea Udaktari | Ordinary diploma in clinical medicine anasoma mtu wa form four na form six wote kwa pamoja. wanaanza NTA level 4 wote kisha NTA level 5 na NTA leve 6.
Hii ni kulingana na mwongozo wa NACTE wa miaka yote kwa sasa. yeyote kati yao akishafika NTA level 5 anaweza kustop na kutunukiwa Technician Certificate au akiendelea na NTA level six basi atatunukiwa hiyo certificate ya ordinary diploma.
Ispokuwa kwa kozi chache za afya (Viungo bandia, biomedical engineering, occupational therapy) Vigezo vya kujiunga kozi za afya katika ngazi ya diploma 2023 ni kuwa na angalau alama D katika masomo ya biology, chemistry & Physics katika mtihani wa kidato cha IV (CSEE).
Hatahivyo, vyuo hutofautiana vigezo/ sifa. Ni vizuri kusoma kwa makini vigezo vya chuo husika ikiwa unataka kuomba kujiunga nacho.
Kozi za Afya: Sifa za kusomea Udaktari
Maabara (Laboratory sciences): Kozi hii itakupa utaalamu wa kuweza kutumia vifaa na vipimo maalum kubaini maradhi, aina za chembechembe katika mwili ambazo hazionekani kwa macho/Kozi za Afya: Sifa za kusomea Udaktari.
Wataalamu wa maabara wamekuwa kiungo muhimu sana kati ya mgonjwa na tabibu.Kwani bila kufahamu aina ya ugonjwa au baadhi ya hali ya kemikali mwilini zilivyo tiba haiwezi kutendeka kwa ufanisi.
Vigezo: Walio na Mtihani wa Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) wenye ufaulu (Alama D) wa masomo manne (4) yasiyo ya kidini ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia/Sayansi ya Uhandisi. Kama una Ufaulu katika Hisabati na Lugha ya Kiingereza unajiongezea nafasi zaidi.
Tiba kwa njia ya mazoezi (Physiotherapy): Hii ni fani ya tiba kwa njia ya mazoezi ili kurudisha utendaji kazi wa viungo baada ya upasuaji au baada ya ajali au kuumwa magonjwa ya aina ingine kwa mdua mrefu.
Kwasasa hali ilivyo, watu wengi sana wanasumbuliwa na maumivu ya mgongo. Wataalamu hawa wa physiotherapia wanaweza kuwatibu kwa haraka bila hata kuhitaji dawa au upasuaji/Kozi za Afya: Sifa za kusomea Udaktari.
Vigezo: Walio na Mtihani wa Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) wenye ufaulu (Alama D) wa masomo manne (4) yasiyo ya kidini ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia/Sayansi ya Uhandisi. Kama una Ufaulu katika Hisabati na Lugha ya Kiingereza unajiongezea nafasi zaidi.
Ufamasia / Madawa (Pharmaceutical sciences): Hii ni moja ya fani ambazo tumekuwa tukiwaona wataalamu wake mara kwa mara.
Wafamasia kwa ufupi tunasema ni wale wanaokupatia dawa hospitali pale unapoambiwa na daktari nenda kwenye dirisha la dawa au hata katika maduka ya dawa.
Kutoa dawa ni kazi moja na huwenda ndiyo ndogo kabisa kwa taaluma hii. Taaluma yao huwawezesha pia kutengeneza dawa, kuchanganya dawa, kusimamia uhifadhi na usambazaji wa dawa pia/Kozi za Afya: Sifa za kusomea Udaktari.
Vigezo: Walio na Mtihani wa Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) wenye ufaulu (Alama D) wa masomo manne (4) yasiyo ya kidini ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia/Sayansi ya Uhandisi. Kama una Ufaulu katika Hisabati na Lugha ya Kiingereza unajiongezea nafasi zaidi.
Utabibu / udaktari (Medicine): Tabibu ni maarufu. Hawa ndiyo wale tunaowaita madaktari. Kazi yao ni kufahamu magonjwa, kuweza kuyachunguza na kuyatibu.
Wako madaktari wa ngazi mbalimbali-diploma (clinical officer), stashahada ya juu (AMO), shahada (Medical Doctor) na daktari bingwa (specialist).
Vigezo: Walio na Mtihani wa Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) wenye ufaulu (Alama D) wa masomo manne (4) yasiyo ya kidini ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia/Sayansi ya Uhandisi. Kama una Ufaulu katika Hisabati na Lugha ya Kiingereza unajiongezea nafasi zaidi.
Uuguzi / Unesi (Nursing): Wauguzi husaidiana na matabibu kutoa huduma kwa mgonjwa. Moja ya kazi za wauguzi ni kuhakikisha mgonjwa kapata dawa, kafanyiwa procedures au vipimo ambavyo ilielekezwa.
Hospitali huwa tunasema kwamba wagonjwa wote ni wa wauguzi kwani huwa nao muda mwingi kuliko mtaalamu mwengine yeyote wa afya.
Kwa wajawazito, kama muuguzi utahitaji kupima ukuaji wa mimba, kumtaarifu tarehe ya kujifungua, na kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto na kumzalisha pindi muda ukifika/Kozi za Afya: Sifa za kusomea Udaktari.
Vigezo: Walio na Mtihani wa Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) wenye ufaulu (Alama D) wa masomo manne (4) yasiyo ya kidini ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia/Sayansi ya Uhandisi. Kama una Ufaulu katika Hisabati na Lugha ya Kiingereza unajiongezea nafasi zaidi.
See also:
Leave a Reply