Kwenda South Afrika sasa ni Bure Kuitazama Yanga SC
Kwenda South Afrika sasa ni Bure Kuitazama Yanga SC – “Tunafahamu Klabu yetu ya Young Africans SC ina mchezo mwingine wa pili kule Afrika Kusini hivyo Uongozi wenu umefanya jitihada za kupeleka Ombi katika Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo chini ya Waziri wetu Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro la kusafirisha mashabiki kwa njia ya Basi na tunaishukuru Wizara kwa kukubali Ombi letu.
Wizara itahudumia gharama zote za safari ya kuelekea Afrika kusini yenye Wanachama na Mashabiki wetu 48 kuanzia Nauli mpaka pesa ya kujikimu, hivyo sisi Young Africans tunaishukuru sana Wizara.
Hapo mwanzo tulitangaza watu watakaosafiri walipaswa kuwa na shilingi laki 6 na tulipata watu 30, niwahakikishie baada ya Wizara kukubali kusafirisha Wanachama na Mashabiki wetu,zile laki 6 zitarudishwa kwa wenyewe.
Niwatakie safari njema na nina imani safari yetu ya kurudi itakuwa nzuri kwakuwa tutarudi tukiwa tayari tumeshafuzu hatua ya nusu Fainali” Rais wa Young Africans SC Eng. Hersi Said akiongea na Wanahabari wakati wa kuwaaga Wanachama na Mashabiki wanaosafiri kuelekea Afrika Kusini Makao Makuu ya Klabu Jangwani.
Rais wa klabu ya Yanga Mhandisi Hersi Saidi amesema Serikali imegharamia gharama zote za Safari ya Mashabiki na Wanachama wa Yanga pamoja na Makundi maalum kuelekea Afrika Kusini Kwa ajili ya mchezo wa Mkondo wa pili wa robo fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi… pic.twitter.com/fd2qR8L7Av
— Prisca Kishamba (@PKishamba) April 1, 2024
See also:
- Matokeo Namungo FC vs Kagera Sugar Leo 02 April 2024
- Vilabu tajiri zaidi barani Afrika 2024 – Transfer Market
- Ratiba ya Simba SC mwezi Aprili 2024 NBC
- Waamuzi wa michezo ya Robo Fainali CAF wiki hii
- Bei ya Magari ya MAZDA ATENZA Tanzania 2024
- Sifa za kujiunga na vyuo vya ualimu ngazi ya diploma 2024/2025
- Sifa za Kujiunga na Chuo cha Utalii 2024
- Sifa za Kusoma Civil Engineering 2023/2024
- Sifa za Kujiunga na Kozi ya Information Technology (IT)
- Paul Makonda ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha
- Sifa za Kujiunga na Chuo cha Mipango Dodoma
- Rostam Azizi kujenga jengo la abiria uwanja wa ndege wa Mwanza
Leave a Reply