Mabondia Waomba Serikali Kuingilia Mvutano wa Azam TV na Amos Mwamakula

Mabondia Waomba Serikali Kuingilia Mvutano wa Azam TV na Amos Mwamakula | Mabondia Waomba Serikali Kuingilia Mvutano wa Kisheria kati ya Azam TV na Amos Mwamakula Kuhusu Mashindano ya “Vitasa”

Septemba 18, 2024, mabondia nchini wameiomba Serikali kuingilia kati mvutano wa kisheria kati ya Azam TV na bondia wa zamani, Amos Mwamakula, ambao umesababisha kituo hicho cha televisheni kujiondoa kuonesha mashindano ya ngumi maarufu kama “Vitasa.”

Mvutano huo ulianza baada ya Mwamakula kudai kuwa yeye ndiye mwanzilishi wa mashindano hayo ya “Vitasa” lakini hakufaidika kwa namna yoyote, licha ya Azam TV kuyatumia kwa miaka kadhaa. Baada ya kufungua kesi, Mahakama iliamuru Azam TV kumlipa Mwamakula Shilingi Milioni 200. Hata hivyo, Azam TV ilikata rufaa dhidi ya uamuzi huo lakini kwa sasa inaonyesha kutokuwa na mpango wa kuendelea kuonesha mashindano hayo.

Mabondia Waomba Serikali Kuingilia Mvutano wa Azam TV na Amos Mwamakula
Mabondia Waomba Serikali Kuingilia Mvutano wa Azam TV na Amos Mwamakula

Mabondia wamelalamika kuwa mvutano huu umeathiri maisha yao kwa kiasi kikubwa, kwani mashindano ya ngumi yalikuwa chanzo kikuu cha mapato kwao, hivyo wanaiomba Serikali kuingilia kati ili kuzuia kudorora kwa mchezo huo nchini.

Mabondia Waomba Serikali Kuingilia Mvutano wa Azam TV na Amos Mwamakula/Wameeleza kuwa maisha yao na ya familia zao yanategemea mchezo huo, na kwa sasa wanakosa jukwaa muhimu la kuonyesha vipaji vyao na kujipatia kipato.

ANGALIA PIA: