Mahitaji ya Kwenda Nayo Kambi JKT

Mahitaji ya Kwenda Nayo Kambi JKT, mahitaji muhimu ambayo vijana wanapaswa kuwa nayo wanaporipoti JKT. Hapa kuna maelezo kamili ya kilichopo kwenye picha hiyo:

Mahitaji ya Kwenda Nayo Kambi JKT

Aidha JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo:

Mahitaji ya Kwenda Nayo Kambi JKT
Mahitaji ya Kwenda Nayo Kambi JKT
  1. Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni, iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
  2. T-shirt ya rangi ya kijani (Green Vest).
  3. Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
  4. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
  5. Soksi ndefu za rangi nyeusi.
  6. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
  7. Track suit ya rangi ya kijani au blue.
  8. Nyaraka zote zinazohitajika katika Udahili wa Kujiunga na Elimu ya Juu, zikiwemo cheti vya Kuzaliwa, Vyeti vya Kuhitimu kidato cha Nne nk.
  9. Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.

Orodha kamili ya majina ya vijana hao, Makambi ya JKT waliopangiwa na maeneo Makambi hayo yalipo na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo, Inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz.

SEE ALSO: