Mambo ya kuzingatia kabla ya kununua bidhaa Mtandaoni (Online): Ununuzi mtandaoni ni kitu ambacho watu hufanya sana miaka hii. Watu hununua vitu kwenye mifumo maalum ya kuuza bidhaa mtandaoni au kwenye mitandao ya kijamii.
Kununua vitu mtandaoni ni jambo zuri na linaweza kufanywa kupitia vifaa kama vile simu au Kompyuta. Moja ya faida za kununua vitu mtandaoni ni kuokoa pesa zako kwa sababu kuna bidhaa zinazopatikana kwa bei ya chini mtandaoni.
Ukiacha faida, kuna mitego ambayo unaweza kukutana nayo katika ununuzi wa mtandaoni. Hapa hatutazungumza moja kwa moja kuhusu changamoto hizi bali tunakupa mambo ya kuzingatia unaponunua bidhaa mtandaoni. Mambo haya yanaweza kusaidia katika baadhi ya changamoto.
Mambo ya kuzingatia kabla ya kununua bidhaa Mtandaoni (Online)
Maelezo kuhusu badhaa
Bidhaa zinazouzwa mitandaoni huwa mara nyingi zinawekwa maelezo ambayo ukiwa kama mnunuzi unatakiwa kuyasoma ili kuielewa bidhaa. Unatakiwa usiishie kuangalia picha na bei tu, hakikisha unasoma na maelezo yaliowekwa kwenye hiyo bidhaa pia. Alafu usisahau kulisoma jina la hiyo bidhaa mara mbili mbili.
Ukiwa na tabia ya kununua vitu mtandaoni bila kusoma maelezo unaweza nunua kitu tofauti na ulichokusudia. Yani badala ya kununua simu, unaweza jikuta umelipia kupata kava la simu.
Angalia maoni toka kwa walionunua
Kabla ya kununua bidhaa Mtandaoni inashauriwa kuangalia maoni kabla ya kufanya maamuzi ya kununua. Mara nyingi watu huwa wanatoa maoni juu ya bidhaa walizonunua mtandaoni na kama bidhaa mbaya au nzuri huwa wanaweka wazi ili wengine wajue. Unaweza ingia YouTube, Facebook au ndani ya platfom unayotumia kununua bidhaa alafu ukaangalia maoni toka kwa walionunua katika kipengele cha “Reviews”.
Hii itakusaidia kujua kitu unachotaka kununua ni vizuri au kibaya. Ila unatakiwa kuwa makini na maoni ya uongo pia. Na fahamu kuwa baadhi ya vitu huwa vinakua vibaya kwa wengine ila ni vizuri kwako.
Utaratibu wa kurudisha bidhaa
Mambo mengi yanaweza tokea baada ya kulipia na kuletewa bidhaa ulioiona mtandaoni. Unaweza letewa bidhaa ikawa haina tatizo, ukaendelea kutumia au ikawa na tatizo, ukataka kurudisha.
Bidhaa ikiwa vizuri ni jambo zuri lakini ukiwa na matatizo alafu ukataka kuirudisha unapaswa kujua kuwa sio kila huduma huwa zinakuruhusu kurudisha bidhaa. Sasa ukiwa kama mnunuzi ambae unaona unaweza chukua bidhaa yenye matatizo kwa bahati mbaya, ni vema ukaangalia utaratibu wa kurudisha bidhaa zenye matatizo kabla hauja nunua hiyo bidhaa Mtandaoni.
Linganisha bei
Badhaa za mtandaoni huwa zinatofautiana bei. Unaweza kuta sehemu flani bidhaa inauzwa kwa bei kubwa kuliko sehemu nyinge lakini ni bidhaa moja. Kutokana na hili, inashauriwa kuwa mtu ambae ukiwa unataka bidhaa mtandaoni, uangalie hiyo badhaa katika sehemu tofauti tofauti na kulinganisha bei. Kwa kufanya hivyo, utapata sehemu ambazo bidhaa unayoihitaji inaizwa kwa bei rahisi.
Usalama wa pesa zako
Unapofanya manunuzi mitandaoni, usisahau kuzilinda pesa zako. Hakikisha unanunua bidhaa mtandaoni katika sehemu inayoaminika ili usiibiwe pesa zako. Hakikisha unajaza taalifa za malipo vizuri ili usije kosea kulipia. Hakikisha haudanganyiki katika kutoa taalifa za akaunti yako ya pesa.
Kama unatumia credit card katika kulipia, epuka kujaza taalifa za Credit card ukiwa umeunganisha kifaa chako na public WiFi bila VPN.
See also:
Leave a Reply