Monalisa Azindua Msimu wa Pili wa Tuzo za WISAC 2024 | Vipengele 30 kwa Wanawake Wanaofanya Vizuri Katika Michezo, Sanaa na Utamaduni.
Mwigizaji Staa, Yvonne Cherrie maarufu Monalisa leo October 30,2024 amezindua msimu wa pili wa tuzo za Women In Sports, Arts and Culture (WISAC) zitakazotolewa kwa Wanawake mahiri Kwenye Tasnia ya Michezo, Sanaa na Utamaduni ambapo ugawaji wa tuzo hizo utafanyika Jijini Dar es salaam November 29,2024 zikiwa na categories 30.
Tuzo hizo ni pamoja na tuzo ya Kiongozi wa kike mahiri kwenye Vyombo vya Habari, pia kwenye michezo, muziki , filamu n.k “Tuzo hizi zinakuja kwa mara ya pili, mwaka huu zitakuwa za kipekee sana tofauti na mwaka jana, tunataka wataoshindania tuzo wawe nyumbani kwao na Familia zao, wawe sehemu za kazi na sehemu yoyote watakayokuwa lakini atafuatilia tuzo hizi kupitia TV, tunataka yule Mama akae nyumbani na Familia yake wamsherehekee pale anapotangazwa umahiri wake katika nyanja anayoifanyia kazi”
Monalisa Azindua Msimu wa Pili wa Tuzo za WISAC 2024
Monalisa amesema watatumia mitandao ya kijamii kuwapa Watu nafasi ya kupendekeza ni nani anastahili kupewa tuzo hizo za heshima “Mwaka jana tulikuwa na vipengele 27, mwaka huu tumeongeza vitatu jumla vitakuwa vipengele 30, mchakato utaanza November 01 hadi Noveomber 11, 2024 ambapo Walaji/ Wananchi wenyewe watapendekeza anayestahili kugombea tuzo hizi kupitia page za Monalisatz, Mwafrikaasilia, Sinema Zetu, AzamTV, ikifika November 12 hadi November 21 tutaanza kupiga kura tukiamini Watu wameshapendekezwa na kila kipengele kutakuwa na Wanaoshindana wanne“
ANGALIA PIA:
Leave a Reply