Mpanzu Kutumika Kwenye Michuano ya CAF

Mpanzu Kutumika Kwenye Michuano ya CAF | Mchezaji mpya wa Klabu ya Simba Elie Mpanzu ataanza kutumika kwenye michezo ya Hatua  ya makundi ya CAF baada ya kukamilisha usajili na miamba hiyo ya soka barani Afrika.

Baada ya vuta nikuvute za muda mrefu kuusu usajili wa kijana huyo raia wa Congo hatimae yametia ya mchezaji huyo kuvaa uzi wa Simba kwenye michuano mbalimbali ambayo klabu ya Simba itashiriki kwenye msimu huu. Mchezaji huyu amekuja kuongeza uhai kwenye eneo la ushambuliaji la Simba SC akimudu kucheza kama kiungo mshambuliaji akitokeo pembeni au katikati ya kiwanja.

Mpanzu Kutumika Kwenye Michuano ya CAF

Baada ya shirikisho kutoa nafasi kwa timu zote shiriki kwenye hatua ya makundi ya mashindano ya CAF msimu huu kufanya marekebisho na maboresho ya wachezaji kwenye mapungufu, sasa inampa rasmi nafasi Elie Mpanzu kuingia kikosini na kuanza kuitumikia klabu yake mpya kuazia hatua ya makundi.

Mpanzu Kutumika Kwenye Michuano ya CAF
Mpanzu Kutumika Kwenye Michuano ya CAF

Vilabu vyote vilivyofuzu kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa ya CAF 2024/25 na Kombe la Shirikisho vina hadi Septemba 30 kufanya marekebisho ya vikosi vyao.

Wanaweza kuondoa au kuongeza mchezaji mpya kwenye orodha waliyowasilisha wakati wa mechi za raundi ya awali. ✅

VIPI KUHUSU LIGI KUU

Mpanzu hatakuwa na kibali cha kucheza mashindano yoyote yanayo andaliwa na TFF kama vile Ligi Kuu NBC, Kombe la Shirikisho la CRDB kwakuwa amesajiliwa baada ya dirisha la usajili kufungwa. Hivyo atapata kibali cha kucheza michuano hiyo punde tu dirisha dogo la usajili la msumu huu wa 2024/25 litakapo funguliwa.

ANGALIA PIA: