MSIMAMO wa Ligi Kuu NBC Leo 27/02/2024 – Msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara NBC baada ya mzunguko wa kumi na saba kuaza.
Katika ratiba ya NBC leo imechezwa michezo miwili katika viwanja tofauti, leo Mtibwa Suagr, Dodoma Jiji, JKT Tanzania pamoja na KMC walishuka uwanjani kutafuta alama tatu kwa kila timu, licha ya nia yao na juudi zilizooeneshwa na timu zote matokeoya mwisho yote ni sare na kugawana alama moja moja.
Ratiba ya NBC Leo na Matokeo yake
Michezo yote imechezwa majira ya saa kumi jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Mtibwa Sugar inayojitafuta kwenye ligi baada ya kuwa na matokeo mabaya kwenye mzunguko wa kwanza waliwakaribisha Dodoma Jiji katika uwanja wa Manungu, Turiani. Mchezo ulimalizika kwa sare ya 0-0 baada ya dakika 90′ kumalizika, hivyo timu kugawana alama moja moja.
Mchezo mwingine ni wa JKT Tanzania walio wakaribisha KMC katika uwanja wao wa Meja General Samuyo, Bunju, mchezo uliomalizika kwa sare ya goli 1-1. JKT goli lao walilipata kupitia mshambuliaji wao Maguli dakika ya mapema sana (08′) na kusawazishwa na Chilunda wa KMC dakika chache kabla ya mapumziko (40′), na kufanya mchezo kwenda sare ya magoli.
MATOKEO | #NBCPL
FT: Mtibwa Sugar 0-0 Dodoma Jiji
FT: JKT Tanzania 1-1 KMC#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #SokaLetuBambam #SokaLetuDamdam #MtibwaSugarVsDodomaJiji #MtibwaSugar #DodomaJiji #MtibwaSugarDodomaJiji #JKTTanzaniaVsKMC #JKTTanzania #KMC pic.twitter.com/42aaGVO8UU
— Azam TV (@azamtvtz) February 27, 2024
MSIMAMO wa Ligi Kuu NBC Leo 27/02/2024
Msimamo bado haujabadilika licha ya michezo hiyo kuchezwa, pengine michezo ya kesho italeta utofauti kwenye msimamo wa ligi ya NBC kwa wiki hii ya 17 ya mzunguko wa pili.
MSIMAMO | Pamoja na kuchezwa mechi mbili leo, bado hakuna mabadiliko katika nafasi tatu za juu katika msimamo wa NBC Premier League.
#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #SokaLetuBambam #Msimamo #Standing #LeagueTable pic.twitter.com/BmUf3TtRZ1
— Azam TV (@azamtvtz) February 27, 2024
See also:
Leave a Reply