MZEE WA MJEGEJE Afariki Dunia

MZEE WA MJEGEJE Afariki Dunia – Msanii wa vichekesho Umar Iahbedi Issa anajulikana kwa jina maarufu la “MZEE WA MJEGEJE” amefariki dunia leo Alfajiri katika Hospital ya Mwananyamala alipokuwa anapatiwa matibabu.

MZEE WA MJEGEJE Afariki Dunia

Meneja wa msanii huyo, Real Jimmy amethibitisha taarifa hizo za kifo cha msanii wake anayekaa Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.

Chanzo cha kifo chake kinatajwa alikuwa anaumwa maradhi ambayo hayajawekwa wazi.

Mzee Mjegeje alikata roho Jumatano asubuhi katika Hospitali ya Mwananyamala iliyo Dar es Salaam, Tanzania alikokuwa akipatiwa matibabu.

MZEE WA MJEGEJE Afariki Dunia

MZEE WA MJEGEJE

Alipata umaarufu wa kimataifa hata nchini Kenya mwaka wa 2022 wakati video yake “kata simu, tupo site” ilipovuma sana kwenye mitandao ya kijamii.

Katika video hiyo iliyomzolea umaarufu mkubwa, msanii huyo wa vichekesho alionekana akiongea kwenye simu ndogo akisema, “Kata simu, kata simu, tupo site. We don’t like disturbance of the head you understand. “

Maneno ya mchekeshaji huyo kwenye video hiyo tangu wakati huo yamekuwa yakitumika katika meme nyingi na hata baadhi ya wasanii wengine wameyatumia kwenye nyimbo zao.

Roho ya Mzee Mjeje ipumzike pema peponi!!!

See also: