Namna ya kuchati na mpenzi wako: Siku hizi kuchati tunaweza sema ndio moja ya vitu watu hufanya sana kwenye simu. Katika muhusiano, mawasiliano ni muhimu sana kati ya wapenzi wanaopenda. Watu wengi wakiwa Katika mahusiano kuchati ndio huwa mawasiliano yao. Kuna watu kwenye mahusiano hutumia app kama WhatsApp,Telegram au huduma za sms za kawaida, kuchati na wapendwa wao.
Namna ya kuchati na mpenzi wako, Yote ni sawa na kuchati ni jambo zuri maana huwaweka wapenzi karibu hatakama wako mbali. Kwa namna nyingine tunaweza sema kuchati huimarisha mahusiano ya mapenzi.
Hapa The bestgalaxy tunaenda kukufungua juu ya namna ya kuchati na mpenzi wako akiwa ni wakiume au wakike. Lakini unapaswa kufahamu kuwa hakuna namna moja ya kuchati na mpenzi, upo huru kuchati na mpenzi wako vile mnavyoona inafaa na inawapa furaha. Ila kama utaona inapendeza au unahitaji msaada, unaweza pia soma yafuatayo ili kujua jinsi au namna nzuri ya kuchati na mpenzi wako.
Namna ya kuchati na mpenzi wako
Weka utaratibu wa kumjulia hali
Salamu au kujuliana hali ni muhimu katika mahusiano na ukiwa unachati na mpenzi wako ni vema ukiwa umeweka utaratibu wa kumsalimia na kumjulia hali. Hii itamfanya mpenzi wako kujua unamjali na umemuweka akilini mpaka unakumbuka kutaka kujua yupo kwenye hali gani.
Unaweza kuwa na tabia ya kumjulia hali mida ya Asubuhi, mchana au muda wowote baada ya kuwa kimya kwa muda. Sio lazima iwe ni kila mara na sio lazima umjulie hali mara chache pia, kikubwa usimsumbue tu/Namna ya kuchati na mpenzi wako.
Maswali au maoini yanaweza kurefusha maongezi
Fahamu mbinu za kurefusha maongezi maana maongezi kuna muda yanaweza kuwa magumu kuyaendeleza. Mnapochati alafu mukafika hatua ambayo maongezi ni magumu kuyaendeleza, Kumbuka kuwa maswali au maoini yanaweza kurefusha maongezi yenu. Muulize maswali kuhusu yeye, vitu anavyopenda na kuhusu mambo mengine. Hii itamfanya awe anajieleza na kufanya maongezi yenu kurefuka. Pia na wewe usiwe mvivu kutoa maoni kwenye majibu yake ili kwenda nae sawa.
Usiwe serious sana mtaishiwa mada
Ukiwa unachati na mpenzi wako, unaweza kuwa na mada nyingi ambazo unaweza ongeanae ili mada hizi ukiwa serious, utaziona hazina maana au zinakera. Kiufupi ikiwa kila unapochati na mpenzi wako unakua serious sana, mambo ya kuongelea yanakua machache sana kiasi ambacho unaweza ukashindwa pata mada kabisa.
Kwaiyo ni vema ukawa haupo serious sana ila mada ziwe zinatiririka kwenye maongezi yenu. Sehemu ya kucheka chekeni, sehemu ya kutaniana tanianeni, sehemu ya kubembelezana bembelezaneni, sehemu za kuongelea ujinga jifanyeni wajinga na kwenye sehemu ya mambo ya msingi ndio kueni serious.
Acha kuchati kabla hamjachoka kuchati
Kama unamtindo wa kuchati sana na mpenzi wako, hakikisha unakua na ujanja huu ili usimkere mwenza wako. Hakikisha ukichatinae sana unaacha kuchati kabla hamjafika hatua ambayo kila mtu amechoka kuchati. Tumia muda wako kuchati na mpenzi wako ila ukiona tu anaelekea kuchoka, acha kuchati nae.
Unaweza katisha maongezi kwa kusema “nitakutafuta baadae kidogo mpenzi wangu” au ukatafuta kisingizio kingine. Kama atakua anataka kuendelea kuchati, kunajinsi anaweza endeleleza mwenyewe maongezi/Namna ya kuchati na mpenzi wako.
Usitume sms nyingi sana anapokua kimya
Ni kawaida kuwa na hali ya kushindwa kujizuia kutuma sms pale mwenza wako anapokua kimya. Ila Hali hii inabidi isikusukume kuwa kero kwa mwenza wako. Ni vema ukiwa kwenye hali hii ukahakikisha hautumi sms nyingi zisizo na maana kwa mpenzi wako. Tuma sms chache zenye kueleweka alafu kama atakua anasoma, atakuelewa na kukujibu.
Mwisho; usisahau kutumia maneno mazuri kwenye kuchati kwenu. Kama muko kwenye mahusiano ni vema mkawa mnachati kama wapenzi na sio marafiki. Kuna muda unatakiwa kuziweka mbali hizo “wewe” “Oya” na kuanza kuzitumia “mpenzi” “mke” “mme” na maneno mengine kama hayo.
Ni hayo tu tulio kuandalia katika ukurasa huu The bestgalaxy, usisahau kuwa karibu na sisi ili kufahamu mambo mengine mengi/Namna ya kuchati na mpenzi wako.
See also:
Leave a Reply