Ratiba ya Kuripoti kwa Wanafunzi wa Kidato cha Tano kwa Mwaka 2024

Ratiba ya Kuripoti kwa Wanafunzi wa Kidato cha Tano kwa Mwaka 2024 | Tarehe Ya Kuripoti Shule Kidato Cha Tano 2024 | Tarehe za Kuripoti Kidato cha Tano 2024

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetangaza tarehe rasmi za kuripoti kwa wanafunzi waliofaulu kuchaguliwa na TAMISEMI kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi stadi kwa mwaka wa masomo. 2024/2025.

Mwaka huu, jumla ya watahiniwa 572,359 walifanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne, huku asilimia 37.42 wakifaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu. Hii inaashiria ongezeko la asilimia 0.47 ya ufaulu ikilinganishwa na asilimia 36.95 ya ufaulu wa watahiniwa wa Divisheni I hadi III, jumla ya 192,348 mwaka 2022. Kati ya watahiniwa waliofaulu, wanafunzi 188,787 wakiwemo 812 wenye mahitaji maalum wamepata nafasi za kujiunga na kidato cha tano katika shule mbalimbali na vyuo vya ufundi stadi kote nchini.

Mchakato huu wa uteuzi umezingatia sera ya elimu na mafunzo ya 2014, pamoja na mtaala ulioboreshwa. Lengo kuu la serikali ni kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi mwenye sifa anapata fursa ya kuendelea na masomo, hasa katika zama hizi za elimu bure/Ratiba ya Kuripoti kwa Wanafunzi wa Kidato cha Tano kwa Mwaka 2024.

Ratiba ya Kuripoti kwa Wanafunzi wa Kidato cha Tano kwa Mwaka 2024
Ratiba ya Kuripoti kwa Wanafunzi wa Kidato cha Tano kwa Mwaka 2024

Ratiba ya Kuripoti kwa Wanafunzi wa Kidato cha Tano kwa Mwaka 2024

Shule za Sekondari: Wanafunzi wa kidato cha tano wanatakiwa kuanza kuripoti shuleni kuanzia tarehe 30 Juni, 2024. Siku ya mwisho ya kuripoti itakuwa tarehe 14 Julai, 2024. Muhula wa kwanza wa masomo ya kidato cha tano utaanza rasmi tarehe 1 Julai, 2024.

Ratiba ya Kuripoti kwa Wanafunzi wa Kidato cha Tano kwa Mwaka 2024, Vyuo vya Ufundi Stadi: Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya ufundi stadi watapata maelekezo ya kuripoti moja kwa moja kutoka katika vyuo husika.

  • Maelezo ya Ziada kuhusu Uchaguzi wa Kidato cha Tano 2024
  • Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa na fomu za kujiunga zinapatikana kwenye tovuti zifuatazo:

Ofisi ya Rais TAMISEMI: www.tamisemi.go.tz Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE): www.nactvet.go.tz
Pia unaweza kutazama orodha ya wanafunzi waliopangiwa nafasi za kidato cha tano na vyuo vya kati kupitia viungo vilivyopo kwenye jedwali hapa chini. Bofya mkoa ulipomaliza elimu yako ya sekondari ili kuangalia shule uliyopangiwa.

ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA
GEITA IRINGA KAGERA
KATAVI KIGOMA KILIMANJARO
LINDI MANYARA MARA
MBEYA MOROGORO MTWARA
MWANZA NJOMBE PWANI
RUKWA RUVUMA SHINYANGA
SIMIYU SINGIDA SONGWE
TABORA TANGA

SEE ALSO: