Sababu za kushindwa kusimamisha uume

Sababu za kushindwa kusimamisha uume: Kuna sababu nyingi zinazoweza pelekea kutokea kwa tatizo la mwanaume kushindwa kusimamisha yaani, kushindwa kuwa na uwezo wa kuamsha uume wake na kuwa imara na mgumu wakati wa tendo la ndoa.

Kuna wanaume hukumbana na tatizo hili kwa muda mfupi au kuwa tatizo la kudumu. Hali hii anaweza kumbana nayo mwanaume wa umri wowote(Mzee au Kijana).

Sababu za kushindwa kusimamisha uume

Sababu zinazoweza sababisha mwanaume kushindwa kusimamisha zinaweza kuwa za kisaikolojia, afya ya mwili, mtindo wa maisha, magonjwa ya zinaa au umri. Hebu tuangaliae zaidi mambo au sababu hizi:

Saikolojia.

Mwanaume akiwa na mfadhaiko, wasiwasi, msongo wa mawazo, au hofu ya kutofanya vizuri wakati wa tendo, anaweza jikuta kashindwa kusimamisha. Yani kama mwanaume hajiamini au mawazo yapo mbali na tendo anaweza kumbana na tatizo hili.

Sababu za kushindwa kusimamisha uume

Afya ya mwili.

Tatizo la kushindwa kusimamisha kwa wanaume wengine linaweza kusababishwa na masuala ya afya ya mwili. Mwanaume akiwa na mwili wenye ugonjwa wa kisukari, shinikizo la damu, matatizo ya moyo, unene uliopitiliza, au ugonjwa wa tezi dume, anaweza kumbana na tatatizo la kushindwa kusimamisha.

Mtindo wa maisha.

Mwanaume pia anaweza shindwa simamisha baada ya uwezo wake wa kusimamisha kuathiliwa na matumizi ya tumbaku, unywaji wa pombe kupindukia, na matumizi ya dawa za kulevya. Pia, kutofanya mazoezi ya kutosha na kula chakula au lishe duni kunaweza kusababisha mwanaume kupata matatizo ya nguvu za kiume.

Magonjwa ya zinaa.

Mwanaume kuwa na baadhi ya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na magonjwa mengine kunaweza muathiri uwezo wake na kupelekea matatizo ya nguvu za kiume.

Umri wake.

Kwa wanaume wengi, umri huathiri uwezo wa uwezo wa kusimamisha. Mwanaume mwenye umri mkubwa anaweza jikuta amepunguza uwezo wa kusimamisha kutokana na umri wake ingawa hali hii huwakuta pia wenye umri mdogo.

Ikiwa mwanaume anasumbuliwa na tatizo hili kwa muda mrefu au mara kwa mara ni vyema kumwona daktari au mtaalamu wa afya ili kupata ushauri na matibabu sahihi yanayoweza saidia kuweka hali sawa.

See also:

  1. Jinsi ya kuangalia mechi za Ligi kuu Tanzania kwenye simu (LIVE)
  2. Dawa YA KUMFANYA mpenzi akupende
  3. Ijue Sayansi ya Ute ukeni, Rangi, harufu na mazingatio yake
  4. Faida za Kiafya za Kufanya Mapenzi Salama
  5. Namna ya kuchati na mpenzi wako
  6. Mambo ya kuzingatia kabla ya kununua bidhaa Mtandaoni (Online)