Sababu za Mwanamme Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa

Sababu za Mwanamme Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa: Ndugu zangu leo napenda tulijadili tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, kwa maneno mengine ya mitaani linaitwa tatizo la kukosa nyege. Tutajadili sababu zinasababisha mwanamme kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, madhara yanayotokana na hali hiyo na kisha kuona ni nini cha kufanya ili kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa au kuongeza nyege.

Bahati nzuri ni kwamba kuna mambo unayoweza kuyafanya kupunguza ukubwa wa tatizo hili au kuliondoa kabisa. Watu wengine wanamini kuwa hamu ya kufanya tendo la ndoa inapungua kadri umri wa mwanamme unavyoongezeka.

Wakati ni kweli kwamba hilo huwatokea wengi, SIYO LAZIMA kwamba hamu ya kufanya mapenzi ipungue umri unapoongezeka. Kuna idadi kubwa tu ya wanaume ambao hamu yao ya kufanya tendo la ndoa imebaki vilevile hata umri wao ulipokuwa mkubwa kabisa.

Sababu za Mwanamme Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa

Mawazo Mengi Na Uchovu

Matatizo ya kikazi na hadhi yako kazini vyaweza kuchangia. Kama unabezwa sana kazini na kujiona hutimizi kazi yako ipasavyo au kama unachoka sana kazini unaweza pia kukosa hamu ya kufanya mapenzi urudipo nyumbani. Kukosa mpango mzuri wa shughuli zako za kila siku na kujaribu kulazimisha kufanya mapenzi katikati ya ratiba yako iliyojaa. Mahusiano ya kimapenzi yanataka yatengewe muda wake na unaotosha.

Msongo Wa Mawazo

Msongo wa mawazo (depression) unatofautiana na kukosa raha au kujisikia si mtu wa thamani kwa kipindi kifupi. Msongo wa mawazo ni ugonjwa wa hali ya kuwa na mawazo makali ya muda mrefu ya kukukosesha raha kutokana na kujisikia si mtu wa thamani au kukosa starehe katika vitu ulivyozoea kuvifanya na kukufurahisha hapo zamani. Mawazo ya namna hii huathiri mwenendo wako wa maisha yako pamoja na matamanio yako ya kimapenzi.

Matumizi Ya Madawa Na Pombe

Matumizi ya baadhi ya madawa na unywaji wa pombe wa kupindukia huweza kuleta tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Madawa yanayochangia tatizo hili ni pamoja na:

– madawa ya high blood pressure
– madawa ya kuondoa msongo wa mawazo
– madawa yote yanayozuia ufanyaji kazi au uzalishaji wa testosterone, kwa mfano, cimetidine, finasteride na cyproterone
– na mengineyo

Umri Kuwa Mkubwa

Homoni ya msingi sana kuhusiana na masuala ya mapenzi huitwa testosterone. Kwa mwanamme homoni hii hutolewa kwa kiwango kikubwa na korodani na kwa mwanamke hutolewa na ovari. Homoni ikipungua katika mwili wa binadamu, humfanya apoteze hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Kiwango cha testosterone katika mwili wa mwanamme hupungua kwa asilimia 1-2 kila mwaka kadri mwanamme anvyozidi kuwa na umri mkubwa. Kiwango cha testosterone kikishuka sana katika mwili wa mwanamme huyu humfanya asiwe na nguvu, ashindwe kutuliza mawazo kwenye jambo alifanyalo na apoteze hamu ya kufanya mapenzi.

Sababu za Mwanamme Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa

Matatizo Katika Mfumo Wa Homoni

Tumeshaona kwamba upungufu wa homoni inayoitwa testosterone unasababisha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Matatizo mengine katika mfumo wa homoni huchangia tatizo hili. Kama thyroid haitoi homoni za kutosha, tatizo hili huweza kutokea ingawa mchango wa thyroid katika tatizo hili ni mdogo sana. Thyroid ni kiungo cha kuzalisha homoni kilichopo katika eneo la shingo.

Tatizo hili linaweza kutokea pale homoni zinapozalisha kitu kinachoitwa prolactin kwa kiwango kikubwa mno na kukisambaza ndani ya mfumo wa damu. Hali hii kiutaalamu huitwa hyperprolactinaemia.

Matatizo Ya Kiafya

Matatizo ya kiafya ya muda mrefu husababisha kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Matatizo ya moyo ya muda mrefu, kuwa na kisukari kwa muda mrefu, kansa ya muda mrefu na hali ya kuwa na unene wa kuzidi kiwango ni baadhi tu ya matatizo yanayochangia tatizo hili.

See also:

  1. Sababu za Mwanamke Kukosa Hamu ya Kufanya Mapenzi
  2. Njia zinazotumika Kuondoa Harufu Mbaya Ukeni
  3. Zijue Dalili za Upungufu wa Nguvu za Kiume na Tiba Zake
  4. Vyakula vya kuimarisha misuli ya uume
  5. Sababu za kushindwa kusimamisha uume
  6. Jinsi ya kuangalia mechi za Ligi kuu Tanzania kwenye simu (LIVE)