Sakata la Kagoma Laibuka Upya, Wataka Kanuni ifatwe

Sakata la Kagoma Laibuka Upya, Wataka Kanuni ifatwe | Yaliyoibuka kwenye Press leo ya Yanga.

Sakata la Kagoma Laibuka Upya, Wataka Kanuni ifatwe — Wakili wa klabu ya Young Africans SC (Yanga), Bwana Simon Patrick, alieleza kwa kina mchakato wa usajili wa mchezaji Yusuph Kagoma katika mkutano na waandishi wa habari. Alionyesha mikataba na kutoa ufafanuzi juu ya hatua mbalimbali zilizochukuliwa na klabu kuhusiana na usajili wake kutoka Fountain Gate FC.

Machi 27, 2024: Yanga SC ilimtumia Yusuph Kagoma tiketi ya ndege, ikiwa ni hatua ya kumleta klabuni kwa ajili ya mazungumzo ya mwisho na kusaini mkataba.

Machi 28, 2024: Kagoma alisaini mkataba wa miaka mitatu (3) na Yanga SC, kuthibitisha uhamisho wake rasmi kutoka Fountain Gate.

Sakata la Kagoma Laibuka Upya, Wataka Kanuni ifatwe
Sakata la Kagoma Laibuka Upya, Wataka Kanuni ifatwe

Aprili 30, 2024: Yanga SC ililipa kiasi cha Tshs 30 milioni kwa Fountain Gate FC kama sehemu ya malipo ya uhamisho wa Kagoma.

Julai 7, 2024: Fountain Gate walituma barua kwa Yanga kuomba malipo ya uhamisho wa mchezaji Kagoma yaelekezwe kwa mchezaji mwingine, Kibabage. Katika siku hiyo hiyo, Yanga SC ililipa Tshs 30 milioni nyingine kwa ajili ya Kibabage.

Hii inadhihirisha kuwa Yanga imefuata taratibu zote zinazotakiwa katika usajili wa Yusuph Kagoma, ikiwemo malipo kwa Fountain Gate kwa wakati.

ANGALIA PIA: