Shughuli za Sanaa Kusimamishwa Kupisha Maulid Zanzibar
Shughuli za Sanaa Kusimamishwa Kupisha Maulid Zanzibar | Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni (BASSFU) limetangaza kusitisha shughuli zote za sanaa na burudani nchini Tanzania kwa muda ili kupisha usiku wa mkesha wa Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W), utakaoadhimishwa Jumapili, tarehe 15 Septemba 2024.
Taarifa hiyo imetolewa kwa mujibu wa Sheria Na. 7 ya Mwaka 2015, ambayo inawapa mamlaka BASSFU kusimamia na kudhibiti shughuli zote zinazohusiana na sanaa, filamu, na utamaduni nchini.
Katika taarifa hiyo, taasisi au mtu yeyote atakayekaidi agizo hilo, atachukuliwa hatua kali za kisheria. Sheria hii inawahusu wasanii, waendeshaji wa kumbi za burudani, na sehemu zote zinazotoa huduma za burudani na sanaa ili kutoa heshima kwa siku hii takatifu.
Kwa hivyo, shughuli zote za burudani nchini, ikiwemo muziki, filamu, na matamasha ya sanaa, zitasitishwa kwa kipindi hicho hadi siku itakapopita.
ANGALIA PIA:
- Simba SC Yapata Sare Dhidi ya Al Ahli Tripoli Ugenini
- Hiki Hapa Kikosi Rasmi cha Simba kinachoaza dhidi ya Al Ahli Tripoli
- WAFUNGAJI Bora NBC Ligi Kuu Tanzania 2023/2024
- Arsenal Imepata Ushindi dhidi ya Spurs kwenye London Dabi
- Jhon Duran Shujaa wa Aston Villa anaetokea Benchi
- Ratiba NBC Championship Tanzania 2024/2025
- Al Ahly Yaanza kwa Ushindi Dhidi ya Gor Mahia
- Ratiba ya Simba Mwezi September 2024 NBC na CAF
- Mechi za Leo CAF Klabu Bingwa Afrika
Leave a Reply