Shule ya Sekondari Kitumbalomo ya Wilaya ya Mbinga

Shule ya Sekondari Kitumbalomo ya Wilaya ya Mbinga | Hii ni shule mpya ya Sekondari Kitumbalomo iliyopo Kata Kitumbalomo Kijiji cha Liwihi Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.

Utekelezaji huu ambao ulifanyika mwaka wa fedha 2022/ 2023 umegharimu shilingi 742,509,99.8 hadi kukamilika na tayari ina wanafunzi wa Kidato cha kwanza ambao walianza masomo mwezi Januari 2024 .

Pamoja na shule hii mpya tayari Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imepokea tena fedha shilingi 560,552,827 kutoka Serikali Kuu kupitia mradi wa SEQIP fedha ambayo itakwenda kutekeleza ujenzi wa shule mpya ya Sekondari katika Kata ya Muungano.

Shule ya Sekondari Kitumbalomo ya Wilaya ya Mbinga

Aidha katika kuboresha mazingira rafiki kwa walimu Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imepokea kiasi cha shilingi 95,000,000 kwa ajili ya kujenga nyumba ya walimu( two in one) katika shule ya Sekondari Kitumbalomo.

Shule ya Sekondari Kitumbalomo ya Wilaya ya Mbinga
Shule ya Sekondari Kitumbalomo ya Wilaya ya Mbinga

Hizi ni jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha inaboresha Sekta ya Elimu nchini.

SEE ALSO: